Brahim Diaz (Man City kwenda Real Madrid).
Mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza, Man City wamejitahidi kuhakikisha mshambuliaji huyo kinda anasalia katika viunga vya Etihad lakini wameshindwa kumshawishi kusalia viungani hapo.
Miamba ya Hispania, Real Madrid imeonesha nia ya kumnasa kinda huyo mwenye miaka 18 kwa dau la paundi milioni 15.5 na mshahara wa paundi 65,000 kwa wiki.
Aaron Ramsey (Arsenal kwenda Juventus).
Dili hili linadaiwa kukamilika kimakubaliano kilichobaki ni kutia wino tu. Kandarasi ya Ramsey na Arsenal inamalizika mwisho wa msimu huu, na sheria zinamruhusu kiungo huyo kutoka Wales kusaini mkataba wa awali na klabu yoyote.
Klabu ya Arsenal hivi karibuni imemuwekea mkataba mpya mezani kiungo huyo , lakini hakuonesha nia ya kubaki Arsenal na kwa sasa yuko tayari kuhamia Italia kwa Vibibi vya Turin Juventus kwa dau la paundi milioni 9 kwa mkataba wa mwaka mmoja akivuta subira hadi mwaka wa pili wa mkataba wake na kujikusanyia paundi milioni 26 kwa msimu nyuma ya staa wao, Christiano Ronaldo.
Ramsey anatarajiwa kutia saini hiyo siku ya kesho.
Dominic Solanke (Liverpool kwenda Bournemouth )
Bournemouth iko mbioni kumnasa Solanke wa Liverpool, japo kwa mkopo lakini kocha wa Liverpool Jurgen Klopp inadaiwa hana mpango wa kumuachia mchezaji huyo na amekuwa muwazi katika hili.
“ Hatuko tayari kumuachia Solanke hata kwa mkopo, na kama atataka kwenda na aende lakini ajue kuwa hatocheza atakaa kwenye benchi tu”
Maneno hayo ni dhahiri kuwa Liverpool haipo tayari kumuachia japo mchezaji mwenyewe anaonekana kuwa tayari kuwaacha majogoo hao wa jiji.
Hirving Lozano. (PSV kwenda chelsea)
Klabu ya Chelsea (the Blues) wako tayari kutoa paundi millioni 26 kumnasa mshambuliaji wa PSV Hirving Lozano.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Mexico atakuwa wa pili kunaswa saini yake na Chelsea baada ya kukamilisha dili la Christian Pulisic kwa paundi million 57.
Hadi sasa, Lozano mwenye miaka 23, ameshafunga magoli 34 katika mechi 64 alizocheza klabuni hapo tangu mwaka 2017. Ujio wa mchezaji huyo ni agizo kutoka kwa kocha, Maurizio Sarri mwenye lengo la kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
Loanee Frank Kessie ( AC Milan kwenda Chelsea)
Chelsea bado wanapigana vikumbo na Tottenham, kuinasa saini ya kiungo wa kimataifa wa AC Milan na timu ya taifa ya Ivory Coast, Loanee kessie.
Kiungo huyo ameonyesha nia ya kujiunga na moja kati ya miamba hiyo ya soka nchini Uingereza. Maurizio Pochetino anamuhitaji kiungo huyo kwa udi na uvumba ili kuziba nafasi itakayoachwa na Mousa Dembele ambaye mkataba wake unafikia ukingoni, na kiungo Mkenya, Victor Wanyama ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha msimu mzima.
Kwa upande wa Chelsea, Kessie anakuwa mbadala wa Cesc Fabregas akisaidiana na usajili mpya Christian Pulisic.
WENGINE
Nathaniel Clyne (Liverpool kwenda Bournemouth) kwenda kwa mkopo na dili limeshakamilika.
Antonio Valencia (Man U kwenda Inter Milan)
Maripan ( Alaves kwenda Barcelona)
Fousseni Diabate (Leicester kwenda Silvasspor)