Taarifa ambazo Kandanda.co.tz imezipata kutoka kwa mmoja wa wanachama wa Klabu ya Yanga, Tawi la Kitunda, zinasema kuwa wamekubaliana kwa kauli moja kuwa hawatafanya uchaguzi ambao umeandaliwa na Shirikisho la soka nchini (TFF) Januari 13 mwakani.
Tamko la wanachama na kwa umoja wetu tumekubaliana kuwa hatutashiriki uchaguzi mkuu wa Tff kwa sababu za ukikwaji wa katiba yanga
Tamko la Tawi la Yanga, Kitunda.
Uchaguzi wa Yanga umepangwa kufanyika tarehe 12/01/2018 baada ya kile kinachoaminika kuwa Mwenyekiti aliyekuwepo, Yusuphu Manji, alijiuzuru. Lakini pia inasemekana baraza la wadhamini wa Klabu hiyo pamoja na kamati tendaji walikataa barua ya kujiuzuru kwake.
Ikumbukwe hivi majuzi akisoma taarifa ya Waziri Mwakyembe kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Ufundi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Yusuph Singo alisema waziri Mwakyembe hafurahishwi na vitendo vya wanachama ambao wamekuwa wakizuia uchaguzi huo ambao yeye aliwatafsiri kama wazuia maendeleo klabu hapo.
Katika taarifa hiyo majina nane yalitajwa kuwa ndio vinara na Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa wanachama hao wanaoongozwa na Bakili Makele, ambapo wanahamasisha wanachama wengine kupinga uchaguzi wa Yanga uliopangwa kufanyika Januari 13, 2019.
Taarifa hiyo imesema kuwa wanachama hao pia wanahamasisha wanachama kususia uchaguzi wakishinikiza kuwa Mwenyekiti wao Yusuph Manji bado yupo madarakani.
Wanachama hao ni:-
Bakili Makele
Mustaph Mohammed
Said Bakari
Shaban Mgonja
Kitwana Kondo
Boaz Kupilika
David Sanare
Edwin Kaisi.
Bakili
ambaye alikuwa Mwenyekiti wa matawi ya Yanga huku Boaz akiwa Katibu wake
walifungiwa kujihusisha na soka miaka mitano na faini ya milioni mbili na
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa kosa hilo hilo wiki kadhaa
zilizopita.