Hakika ilikuwa ni vita kati ya ‘Gegenpressing’ ya Jugen Klop dhidi ya ‘Tik tak’ ya Pep Guardiola, pamoja na kuonekana kama ni aina ya uchezaji unaofanana lakini kuna utofauti mkubwa wa ‘patterns’ za uchezaji ndani ya kiwanja huku zote umiliki wa mpira ukiwa ndio msingi mkuu
Klop anayetamba na Gegenpressing yake aliingia kwenye mchezo dhidi ya City akifanya mabadiliko ya mfumo kutoka ule wa 4-3-3 na kwenda kwenye mfumo wa 4-2-3-1 hii ndio sehemu ya kwanza aliyoweza kuishinda City kwa maana huu ni mfumo ambao mara nyingi hutoa uwiano sawa kwenye kujilinda na kushambulia pia kuua muunganiko wa kimbinu wa mpinzani kutokea katikati ya kiwanja pia ni flexible formation kurudi kwenye 4-3-3
Kwa kuwapanga Emre Can na Giorgio Wijnaldum kucheza pamoja kwenye eneo la kiungo, hii iliweza kuifanya safu ya ulinzi ya Liverpool kuficha makosa mengi ambayo mara nyingi huighalimu timu hapa Klop alifanikiwa kukata mawasiliano ya viungo wa City na safu ya ushambuliaji, lakini pia iliifanya safu ya ushambuliaji kupata mipira kwa wakati hasa pale wanapokwenda kwenye counter attacking tactics
Oxlade Chambe, Mohammed Salah na Sadio Mane hakika wameonesha kitu kilekile ambacho huwa wanakifanya shooting, movements, attacking tactics, counter attacking tactics na kasi kwenye ushambuliaji bado Salah aliweza kulifanya eneo hili kuwa bora sana
Kupunguza umiliki wa mpira hakika hii ni mbinu nyingine ambayo Klop alifanikiwa katika kuiangamiza City kwa maana iliongeza ubora kwenye attempting possession
Pep Guardiola aliingia na mfumo wake uliozoeleka wa 4-3-3 huku umiliki wa mpira ukiwa ndio silaha yake, lakini tatizo kubwa likiwa katikati ya kiwanja maala ambapo Liverpool waliweza kuziba njia za mipira
Kuufa kwa muunganiko wao wa kimbinu kutokea katikati ya kiwanja kuliifanya City kushindwa kufikisha mipira kwenye eneo la 14 zone hapa ndipo hujenga mashambulizi yao Ilkay Gundorgan, Kelvin De Bruyne na Fernandinho walioneka kuzidiwa mbinu na viungo wa Liverpool
Safu ya ulinzi
Hakika hili ni eneo ambalo City hawakuwa bora katika mchezo wa leo, walifanya makosa mengi yaliyopelekea Liverpool kuyatumia vema kujipatia mabao, kushindwa kujipanga kwa wakati ili kuendana na kasi ya washambuliaji wa Liverpool ni aina ya makosa ambayo yameigharimu timu
Fabien Delph, John Stones, Kyle Walker na Otamend walionekana kuhitaji msaada mkubwa kutoka kwa viungo wao wa kati
Yote kwa yote Liverpool wameendeleza rekodi yao ya kutofungwa na Manchester city kwenye ardhi yao, huku Klop akifanikiwa kumsimamisha Pep baada ya michezo 30, bila kupoteza