Kwa hakika ulikuwa mchezo mzuri na wenye ushindani wa kiufundi kwa timu zote mbili.
Simba wakitumia tactical deployment 3-5-2 walionekana kumiliki mpira kwa kiasi fulani kuanzia kwenye eneo lake la kiungo, tofauti na michezo iliyopita kwenye mchezo wa leo simba walionekana kuimalika vema kwenye mfumo na aina yao ya uchezaji.
Juuko murshid, Erasto nyoni na Asante kwasi walionekana kucheza kwa utulivu mkubwa kwenye safu ya ulinzi, huku wakipata msaada mkubwa kutoka viungo wao wa kati.
Kwenye safu ya kiungo kwa hakika hapa ndio palikuwa silaha ya Simba kwenye mchezo wa leo, Jonas mkude, Mzamir yasin na James kotei walikua na muunganiko mzuri sana wa kimbinu na aina ya uchezaji wa pasi fupifupi kwenye kipindi cha kwanza high speed pass, pass combination na pressing tactics walikuwa vizuri sana hata kuingia kwa Said Ndemla alikwenda kuwapiteza kabisa Mudathir Yahya na Tafadzwa Kutinyu waliokua eneo la kiungo kwa upande wa Singida United. Sehemu ya kiungo ndilo eneo ambalo Simba walilitumia kuamua mchezo wa leo.
Hata pale ambapo Simba walibadilisha aina ya uchezaji kwenda kwenye long balls bado eneo la kiungo la Simba lilisimama na kuendelea kucheza katika ubora uleule.
Safu ya ushambuliaji ya Simba hakika leo wakicheza kwa ubora mkubwa na wa hali ya juu. Tumeweza kuona kasi ya kama mshambuliaji aliyoionyesha Shiza kichuya, counter attacks na finishing ya Emanuel okwi, ambae ameonesha kuwa yeye ni clinical finisher akitokea benchi anakwenda kufunga mabao mawili. Pengine kukosa umakini kama sio bahati kwa nahodha John Bocco kungeifanya Simba kuondoka na ushindi mnono zaidi ya mabao manne.
SINGIDA UNITED
Hakika leo hawakuwa kwenye kiwango bora, maeneo mengi walionekana kupwaya sana.
Tofauti na michezo iliyopita, leo safu yake ya ulinzi ilionekana kukosa muunganiko mzuri wa kimbinu, Kennedy Juma na Malik Antir waliokosa maelewano kabisa kama mabeki wa kati, kushindwa kujipanga. Pia mabeki wa pembeni Shafiq Batambuze na Michael Rusheshangoga kushindwa kufanya pre marking ni makosa ambayo yamechangia kupoteza mchezo wa leo kwa idadi kubwa ya mabao.
Eneo lake la kiungo hili naweza kusema kwa kiasi kikubwa lilionekana kuiangusha timu kwa kiasi kikubwa. Hans Van Plujim anajulikana kwa kujua kusuka sehemu ya kiungo katika timu zake lakini leo timu ilikosa muunganiko mzuri kuanzia eneo la kiungo wa chini alipoanza nahodha Mudathir Yahya ambae alishindwa kucheza kama kiungo halisi wa ukabaji. Ilionekana mapema Tafudzwa Kutinyu sio aina ya kiungo ambaye anaweza kushinda vita katikati ya uwanja kuonekana hayuko timamu kimwili na pia aina ya viungo wa Simba walivyokua wanacheza leo.
Eneo la ushambuliaji kidogo walionekana kuisumbua safu ya ulinzi Simba. Kukosa kwa nafasi za wazi na umakini kwa washambuliaji Lubinda Mundia na Papaa Kambale kuliifanya Simba iondoke uwanjani bila wavu wake kutikiswa. Pia tatizo kubwa likiwa aina ya mipira waliyokuwa wakipewa na viungo wao kutokea sehemu ya katikati ya uwanja (high balls) pia kufa kwa eneo la kiungo kulipelekea safu hii kuzorota huku Kambale Salita ambaye alicheza kama mshambuliaji wa pili ama kiungo wa juu akishuka sana chini kufata mipira, hii ilifanya kukosekana kwa mtu wa kuratibu pasi za mwisho.
Pamoja na yote lakini uteuzi wa mfumo, upangaji wa kikosi na game plan waliyoingia nayo Singida United vimechangia kuingusha timu hii na kupokea kipigo kizito.