Kipa wa Uganda na nahodha, Denis Onyango, ameionya Tanzania kuwa Cranes imedhamilia kudumisha mbio zao za kuwania kufuzu kombe la mataifa ya Afrika 2019 bila kupoteza, wakati majirani hao wakikutana Dar es salaam Machi, 24
Taifa Stars, inahitaji kushinda mechi hiyo ya mwisho ya kampeni huku wakitegemea Cape Varde waisimamishe Lesotho ili ipate nafasi kutoka kundi L kwa fainali za mwaka huu
Uganda, tayari imefanikiwa kuvuna alama 13, wakati Lesotho na Tanzania zina alama 5 na Cape Verde ina alama nne
“Tunakwenda Tanzania kwa lengo la kushinda, tunajua kua Tanzania wanahitaji ushindi ili kufuzu, lakini tumeamua kumaliza bila kufungwa.
Onyango, ambaye hivi karibuni alisaini mkataba wa miaka minne na klabu yake ya Mamelodi Sundowns, amecheza bila kuruhusu goli katika mechi zao 5 za kufuzu Afcon.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, amekua na majeraha ya goti lakini anataraji kurejea katika mchezo huo mkubwa Afrika Mashariki
“Nataka kutengeneza historia ya kutoruhusu goli katika mechi za kufuzu kwa sababu hiyo inamaanisha mengi kwangu”
“Lakini sio kazi rahisi sana kucheza dhidi ya Tanzania kwa sababu wanatujua vizuri” aliongeza Onyango
Tanzania inahitaji kufuzu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980, huku Uganda wao wakirejea baada kushiriki fainali zilizofanyika Gabon 2017.