Sambaza....

Mara kwa mara tumekua tukilalamika  katika nchi yetu kukosa washambuliaji  halisi wenye ufasaha  mkubwa katika  kumalizia nafasi za wazi na kufunga magoli.  Huku wengine wakikiri kabisa kua hatuna washambuliaji halisi wanaoweza kusimama kama namba 9 na kufanya kazi ya kufumania nyavu tuu.

Pengine sasa ni wakati wa kugeuza fikra zetu na kuamini katika tulichonacho na kukifanya kiwe bora kwa manufaa ya klabu zetu na timu ya Taifa.

Kwa sasa Watanzania tunatakiwa kujivunia hali ilivyo haswa katika eneo la ushambuliaji kwa sababu kuu mbili. Yakwanza ni katika Ligi Kuu Bara katika orodha ya wafungaji na ya pili ni wingi wa washambuliaji wa Tanzania kuhitajika nje ya nchi.

1. Katika Ligi Kuu Bara

Orodha ya wafungaji katika TPL mpaka sasa imetawaliwa na wazawa wengi huku wageni wachache nao wakikomaa. Anaeongoza kwa ufungaji wa mabao mpaka sasa ni Salim Aiyee anaetokea katika klabu ya Mwadui akiwa na mabao 13 akifwatiwa na Heritier Makambo(Yanga) na Meddie Kagere (Simba sc) wenye mabao 12.

Lakini chini ya vinara hao watatu kuna wazawa wengine ambao nao wanakomaa katika ufungaji wa mabao huku wakiwa katika nafasi nzuri za kuendelea kupachika mabao kama ambavyo orodha inaonyesha.

Kwa chati hii ya ufungaji wa mabao ni wazi bado washambuliaji wetu wa nyumbani hawapo pabaya na wana  nafasi kubwa ya kuibuka na kiatu cha dhahabu.

Ayoub Lyanga mshambuliaji wa Coastal Union

2. Washambuliaji wa Tanzania kuhitajika nje.

Wakati sisi wenyewe (Watanzania) tunaamini washambuliaji wetu ni butu katika kufumania nyavu imekua ni kinyume na watu wa nchi za nje wanavyowaona washambuliaji wetu. Kumekua na wimbi la washambuliaji wetu kutakiwa na vilabu vya Africa na Ulaya pia.

Pengine kufanya vizuri kwa Mbwana Samata akiwa Krc Genk kumefungua njia kwa vijana wetu:

Shabani Idd Chilunda – CD Tenberife

Yahya Zayd – Ismailia (Misri)

Eliudi Ambokile – Black Leopard (Africa Kusini)

Simon Msuva – Difaa El-Jadida (Morroco)

Rashid Mandawa – BDF-11 (Botswana)

Hao ni baadhi ya washambuliaji ambao wameonekana wanafaa katika nchi za nje achana na wengine ambao wamekua wakienda kufanya majaribio kama kina Kelvin Kiduku aliekua Africa Kusini na pia tunaambiwa Habibu Kyombo msimu ujao atakua na kikosi cha Mamelody Sundows nchini Afrika Kusini.

 Hitimisho

Wachezaji wote hao wanaonekana wakiwa katika viwango vizuri kwa sasa tatizo ni moja tuu. Washambuliaji wetu wengi hawana “Consistency” msimu mmoja au miwili atakua kwenye kiwango bora baadae anapotea kabisa na kushindwa kulinda uwezo wake kama kina Hussein Javu, Said Bahanuzi, Jerry Tegete na wengine wengi.

John Bocco akipambana na Andrew Vicent

Kwa washambuliaji wetu wa Tanzania ni John Raphael Bocco pekee alieweza kistahimili katika kiwango chake kwa muda mrefu (zaidi ya miaka 10). Pengine vijana hawa chipukizi ni vyema wangekaa na kaka yao awaelekeze nini chakufanya.

Eliud Ambokile, Shabani Chilunda, Vitalis Mayanga, Yahya Zayd, Ayoub Lyanga, Salim Aiyee, Said Dilunga na Habibu Kyombo ni  vijana wadogo wakiwa chini ya miaka 25 hivyo ni vyema tukawasaidia wakue katika misingi mizuri ili wasipotee katika ramani ya soka iwe hazina kubwa kwa Taifa.

Sambaza....