JKT Queens ambao wamechukua ubingwa bila kupoteza mchezo hata mmoja sasa watahamishia nguvu zao katika michuano ya kanda ya Cecafa ili kupata mwakilishi ambae atakwenda kuiwakilisha kanda hii katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Endapo watanyakua ubingwa huo maana yake watakua wamewalipa kaka zao wa JKT Tanzania ambao wametwaa ubingwa wa Ligi ya Champioship na kurudi Ligi Kuu.
Vihiga Queens kutoka Kenya ilikua bingwa kwa mara ya kwanza mwaka 2021 huku Simba Queens ya Tanzania ikishinda mwaka jana
Mchezo huo wa watani wa jadi unatarajiwa kuwa wa kuvutia kutokana na ushindani uliopo baina yao na matokeo ya sare katika raundi ya kwanza.
Simba Queeens wanakwenda kukutana na Yanga Princess wakiwa kileleni na alama 26 sawa na Fountain Gate lakini wao wakiwazidi magoli. Yanga Princess wao wapo nafasi ya nne wakiwa na alama zao 21.
Tayari klabu yake ya Simba juzi ilishatoa taarifa rasmi yakumtakia kila lakheri nyota wao huyo aliyefanya vyema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwepo katika kikosi bora cha mashindano
Simba na Yanga wakiwa ugenini wameshindwa kabisa kujitutumua na hivyo kuangukia pua katika michezo yao ya raundi ya pili.
Mchezo huo unategemewa kuwa na ushindani mkubwa kwani timu hizo zinafuatana katika msimamo wa Ligi
Opa aliiongoza timu yake ya Simba Queens kufika nusu fainali ya Ligi ya mabingwa ya wanawake Afrika waliposhiriki kwa mara ya kwanza msimu uliopita.
Shambuliaji huyo ambae pia ni nahodha wa Simba ameendela kuuwasha moto katika Ligi hiyo tangu ilipoanza na kuonekana ameongezeka makali kutoka na uzoefu mkubwa alioupata katika Ligi ya Mabingwa Afrika