Haya ni maoni ya shabiki wa Kandanda, karibu usome na tupe maoni yako pia.
Dhana ya kutokuwa na hatia ni kanuni ya kisheria ambayo mtu huchukuliwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe na hatia
Nimemsikiliza kwa makini sana Bwana Mdogo Ramadhani Kabwili kupitia audio zilizozagaa kwenye Makundi Sogozi siku nzima ya leo, nikakumbuka Mwaka 2015 nilipata wazo la kuandika Tafiti ya Kisayansi (Scientific Research) juu ya suala la Upangaji wa Matokeo kwenye michezo ya Ligi zetu kuanzia ya juu kabisa Premier League hadi ya chini kabisa daraja la nne maana huko mtaani kumekithiri maneno ya namna hiyo kila Timu fulani ikishinda huwa ni kwamba Wamenunua Mechi ama kwa kuwahonga Waamuzi ama Kununua wachezaji wa timu pinzani na kwa hili huwa linatokea mara nyingi kwa Vilabu vyetu viwili vikubwa sana hapa nchini pindi wanapokuwa na Neema ya Rujwaa, Furusi, Fedha, Hela!
Na kuhusu Tafiti yangu ile nilikuwa nishaandaa hadi Dhima Maalum kabisa (Specific Objectives) za kwenda kufanyia Tafiti ile ambayo ingekuwa imejikita katika Namna ya Tafiti za kivumbuzi (Exploratory Research) miongoni mwa sababu ambayo ilisababisha niishie njiani ni Upatikanaji wa Taarifa za Msingi kwa maana ya (Primary Data) nani angekuwa tayari kutoa Taarifa ama ndio ningeifanya katika Mtindo wa Kukusanya Taarifa kama Observer yule wa Siri (Participant Observer kwenye namna ile ya Covert) ama (Non participant observer) ila changamoto nyingine ilikuja kwa mawazo yangu ni kwamba Tafiti za namna hii zilizolalia kwenye Empirical Studies zinahitaji sana Rejea (Refernces) kutoka Sehemu husika ningeweza kukopa toka Kwenye somo lile lililoishusha Daraja Juventus kutoka Serie A hadi Serie C plus makato ya Alama 18 kwenye ile kashfa ya Calciopoli ama hata Nchi Jirani nyingine ambazo kwa maana moja ama nyingine zina hizo Empirical Studies lakini ningekosa Rejea kutoka eneo husika maana ili kuweza kufanya Empirical studies unahitaji Empirical literature review najua Para hii watanielewa wachache sana maana nimeshindwa kuiweka kwa Kiswahili chepesi nieleweke!
Leo hii Inawezekana kuna akina Kabwili wengi sana wanatamani waongee hizi kitu lakini hawana pa kuongelea/ hawana Uthubutu/ wanaona bora tu waache yaende/ maana kesi za namna hii huwa ni mbaya sana kwa pande zote aidha Mchezaji upotee kabisa kwenye mpira pamoja na kifungo Jela ama Club ishushwe Daraja na kupokwa baadhi ya mataji yake jumlisha na Alama zake kwenye ligi watakayopelekwa huko hii ina maana Kesi hii si ndogo japo huko nyuma kulikuwa na kesi kama hii kuwahi kutajwa na Kipa Shaaban Kado akiwatuhumu Viongozi wa Simba Sports Club kumtumia Mchezaji wao wa Zamani kwenda kumpenyezea Mlungula na yeye (Kado) akamripoti kwa Viongozi wake wa Mtibwa lakini nani anaaikumbuka Kesi ile? Nana anajua iliishia wapi? Kitu pekee hadi naandika haya Kado bado anacheza Mpira tena wa Ushindani hadi sasa pale pale Mtibwa Sukari Football Club wakijiita Bavarians wa Manungu!
Kipekee tu niseme huu ndio Wakati ambao kama Taifa tunapaswa kusimama Imara na kupitia Vyombo stahiki Uchunguzi stahiki Ukafanywa kubaini je kuna Ukweli juu ya Tuhuma hizi za Kabwili dhidi ya Simba Sponga? Ama alikuwa anaongea ongea tu kupitisha muda kwenye Kipindi cha Redio alichoitwa kwa mahojiano na kama Zina Ukweli basi Hatua Stahiki zichukuliwe na kama Hazina ukweli basi Hii tabia Ikomeshwe maana iliachwa kwa Kado na sasa kwa Kabwili kama itaachwa itamea na kukua miongoni mwa Wachezaji huku ikiendelea kuleta Kadhia kwa sisi wapenda Soka!
Mwisho tu nitoe angalizo kwa kusema kama kuna Wakati ambao Wapenda Mpira wa Nchi hii tunapaswa kusimama pamoja ni kipindi hiki hasa kwenye HII KASHFA MBAYA INAYOUNAJISI MPIRA WETU kipindi hiki cha sasa inatupasa kuzika TOFAUTI ZETU na kupigana vita kali dhidi ya hizi kelele za Rushwa michezoni kwa namna yoyote ile kama zipo basi wahusika wapelekwe kitanzini na ama kama hazipo basi wanaozitaja wachukuliwe hatua kali sana za kisheria ili wasizitaje tena ama kuvihusisha Vilabu vyetu na KASHFA za namna hii Rejea wazo langu pale juu la Kutaka kufanya Tafiti ya Kisayansi (Scientific Research) juu ya Rushwa michezoni, nia nilitaka kuleta majibu ya Kisayansi ili nisaidie Taifa katika kuondoa Rushwa Michezoni!
Mwisho kabisa niseme tu Tumuombee Ramadhani Kabwili nasema Tumuombee Ramadhani Kabwili maana anatuhitaji kwa Maombi kuliko kipindi chochote cha Career yake ya Mpira maana hapa anaweza kuwa amejiua yeye mwenyewe na Kufutika kabisa kwenye Ramani ya Soka ama Kuandika Historia mpya kabisa ya Mpira kwenye Nchi hii ikiwa tu maneno aliyoyasema leo yana Ukweli pasi na Chembe ya Mashaka!
Tumuombee huyu Mtoto maana kama yeye ndio kaamua kumfunga Paka Kengele basi tumpe Support yetu kwa Umoja wetu maana kama kuna muda Ramadhani Kabwili anawahitaji wapenda Mpira wa Nchi hii ni muda huu ila tu kama tunaupenda mpira ila kama tutatanguliza rangi za Jezi za Vilabu vyetu mbele kabla ya Maslahi mapana ya Mpira basi tuachane na Mpira wenyewe!
Wito wangu tu kwenu Wapenda mpira Tusiishie kuwa Keypad Warriors tusiishie kupigana hii VITA kwa kumtazama Kabwili kama Adui tusimtie hatiani hadi pale atakapokuwa na Hatia ya kujibu!
©️Mdidi the Writer ?