Sambaza....

Hakika Afrika ina kila sababu ya kujivunia kuwa na Kocha wa aina ya George Lwandamina “Chicken”, Ni mtu mwenye kariba ya Upole na utaratibu pamoja na utu uliopindukia lakini ndani ya kichwa chake kuna madini ya ujuzi wa ajabu katika Mpira wa miguu, Ana leseni A UEFA ya ukocha, Ukocha Amesomea Ujerumani pamoja na Uholanzi

HEKIMA , UTU NA USTAARABU AMBAO ANAO

Ni kweli kabisa Yanga inapitia katika hali ngumu ya Kiuchumi lakini kwake Lwandamina hiyo siyo sababu yakumfanya Ashindwe kufanya kazi ndani ya Klabu ya Yanga, Nakumbuka Yanga walikuwa na Malimbikizo ya Mshahara wa Kocha, alikuwa hajalipwa takribani miezi minne, lakini siku ilipopatikana pesa na uongozi kutaka kumlipa kocha huyu, Nakumbuka Lwandamina alikataa nakusema hiyo pesa walipwe wachezaji kwanza yeye ana tatizo atavumilia tu, Hakika hii ni busara, na hekima iliyopitiliza

Image result for Lwandamina

Lwandamina ni aina ya kocha ambaye hapendi kuwa na wachezaji ambao wanaelea tu, Anaamini kuwa ukimuona mchezaji anaelea ujue ameundwa so siku zote anapenda kuwa na wachezaji ambao anawatengeneza yeye mwenyewe kwa mkono wake kisha wanakuwa Bora, HAPA NISISITIZE, kwa wachezaji wa Yanga ambao chipukizi ikitokea wakashindwa kucheza mpira wakiwa mikononi kwa Lwandamila basi wafahamu kuwa wachezaji hao watahitajika kujibadirisha sana na kufanya kazi ya ziada ili wacheze siku za usoni, Lwandamina amekuwa mzazi na amekuwa kama Mlezi wa Wachezaji ndani ya Yanga

Siku zote ana misemo miwili mikubwa anapenda sana kuiongea Lwandamina katika falsafa zake za Mpira wa miguu

Anapenda kusema (1) “Anapenda kusema hakuna kitu kizuri kanachotokea tu, ni lazima kitengenezwe kwa misingi sahihi” Hapa Mr Chicken anatuambia wapenda Soka kuwa Wachezaji wazuri hawatokei tu bali wanatengenezwa lakini pia anamaanisha Timu mzuri aitokei tu bali inatengenezwa pia, Ni sawa ata kwenye maisha yetu yakawaida ya kila siku, Maisha Mazuri ayatokei tu bali yanatengenezwa…

Msemo wa pili anapenda kusema Kila jambo linaweza kufanyika vizuri endapo utakuwa na moyo wa upendo, uvumilivu na uwazi, Huyu ndiye Lwandamina nani anaweza kataa maneno yake haya ya hekima? Ni mwalimu gani anaweza kufundisha mwanafunzi wake pasipo upendo na Mwanafunzi akaelewa somo? Mwalimu gani anaweza kufanya kazi pasipo uvumilivu? Mwalimu gani ataeleweka kwa Wanafunzi kama hana Uwazi?

Mpango mkakati wake kwenye mpira

Ni aina ya kocha ambaye anaangalia katika ushindi zaidi, Siku zote Lwandamina anakuambia haina Maana kwa kocha yeyote bora kuwa na 80% za kumiliki mpira uwanjani lakini mwisho wa siku matokeo unapoteza mchezo, anasema jambo la kwanza katika mpira ni kutafuta Ushindi kwanza ndicho kinachoangaliwa na kila mmoja

Hapa alinifungua akili ya soka nakumbuka huu ugonjwa Tanzania tunao sana, kipindi cha kocha Marcio Maximo akiwa Timu ya Taifa nakumbuka Timu kubwa kubwa kutoka nje zilikuwa zinakuja na tulikuwa tunacheza nao na kuwadhibiti sana na kila mmoja akitoka uwanjani anasema tumecheza sana mpira leo na tunatamba kuwa jamaa tunawamudu kabisa lakini mwisho wa siku majibu yanabaki pale pale kuwa tunefungwa umiliki wetu wa mpira hautusaidii ,Lwandamina anafanya na kazi kubwa sana, Kwanza kujenga saikolojia ya wachezaji waweze kupambana uwanjani lakini pia kuandaa mikakati ya kiufundi uwanjani pasipo kuwa na three key players ambao ni Kamusoko, Ngoma, na Tambe…..Hakika inakuwa kazi ngumu kwake
hiyo ndiyo tunaita Result team orien

Wanayanga na wapenzi wa soka nchini wanahitaji kumpa mda wakutosha mtaalamu huyu ipo siku watakula matunda pasipo shaka, endapo Lwandamina angekuwa Mzungu nina uhakika leo hii asingekuwa Tanzania kutokana na uwezo wake wakufundisha soka

Hiyo ndiye George Lwandamina nguzo ya chuma iliyobeba taa zenye mwanga wa dhahabu ndani ya kikosi cha Yanga sc

Sambaza....