Sambaza....

Klabu ya soka ya Sunderland imevunja mkataba na mlinzi Papy Djilobodji baada ya kuchelewa kuripoti kambini pamoja na kurudi akiwa hayupo timamu kimazoezi (Kupungua uwezo wa kusaka kabumbu).

Papy Djilobodji mwenye umri wa miaka 29 ambaye alikuwa akiichezea Dijon kwa mkopo msimu uliopita aliwahi kuomba kundoka klabu hapo na mwezi Juni aliandika barua ya kuomba kuondoka mazima na kuangalia utaratibu mwingine.

Lakini alishindwa kuripoti mapema klabuni hapo na kuanza mazoezi na wenzake mwezi Agosti baada ya Sunderland kumruhusu kwenda likizo isiyo na malipo ili aweze kushughulikia makubaliano yake na klabu yake mpya (ambayo haijatajwa).

Klabu hiyo imeeleza kuwa aliporudi alishindwa mtihani wa utimamu wa mwili na pia alichelewa kuripoti hali iliyoilazimu bodi ya klabu hiyo kufikia makubaliano ya kuuvunja mkataba wake.

Mkataba wa Djilobodji ulikuwa unafikia Tamati Juni mwaka 2020 na alirudi kambini Juma la kwanza la mwezi Septemba baada ya kudharau matamko mbalimbali ya klabu hiyo ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza nchini England (League One).

Djilobodji alisajiliwa Agosti mwaka 2016 ukiwa ni usajili wa kwanza wa Meneja David Moyes akitokea kwa mkataba wa Paundi Milioni 8, lakini mara ya mwisho kuichezea timu hiyo ilikuwa ni Agosti mwaka jana.

Sambaza....