Mshambuliaji wa timu ya soka ya Liverpool ya Uingereza Daniel Sturridge amekutwa na hatia ya kuvunja kanuni za kubashiri cha chama cha soka England.
FA imesema katika taarifa yao kuwa kitendo hicho kimetokea mwezi Januari mwaka huu, ambapo Sturridge anatuhumiwa kuvunja kanuni inayokataza kutoa taarifa za wachezaji, viongozi, uchaguzi wa timu kabla ya muda wake sahihi.
Kifungu hicho kinakaza kabisa kwa mchezaji kutoa taarifa za timu kwa lengo la kutumika kwenye michezo ya kubahatisha na endapo itafahamika kukiuka basi hatua kali zitachukuliwa kwa mchezaji, kocha au kiongozi yeyote wa klabu.
Hata hivyo klabu ya Liverpool kupitia kwa msemaji wao imemtetea Sturridge kwa kusema kuwa wanaamini hawezi kufanya hivyo kwani hajawahi kuhusika katika aina yoyote ya michezo ya kubahatisha na wanaamini atatoa ushirikiano ili kufanikisha uchunguzi unaoendelea.
Sturridge mwenye umri wa miaka 29 amepewa muda hadi Novemba 20 kujibu tuhuma hizo ama kukubali au kukataa ili FA iweze kumpa adhabu kwa kitendo hicho.