Yanga imeanza kuisuka tena timu yao baada ya kuanza kusuasua na katika michezo ya VPL na na kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Baada ya kukimbiwa na kuvunja mikataba na nyota wake wa kigeni Juma Balinya na Sadney Urbrok katika eneo la ushambuliaji sasa wameamua kuziba nafasi zao ili kuweka mambo sawa.
Ikumbukwe katika usajili wa dirisha kubwa msimu huu Yanga ilikua imesajili washambuliaji wa kigeni tupuu huku kukiwa hakuna mzawa hata mmoja.
Tariq Seif ni kijana chipukizi anaekuja vizuri katika eneo hilo huku akionyesha umakini mkubwa katika kufumania nyavu, akionyesha hayo alipokua katika vilabu vya Stand utd na Biashata utd.
Baada ya msimu wa 2018/2019 kumalizika Tariq Seif alipata bahati ya kwenda nchini Misri katika klabu ya Derkens lakini Yanga wakaona wamrudishe nyumbani ili aweze kuwasaidia katika VPL na kombe la FA.
AIOKOA BIASHARA ISISHUKE DARAJA.
Baada ya kuanza vibaya baada ya kurejea Ligi Kuu baada ya miaka 10 timu ya Biashara ilikua katika hatari ya kushuka daraja na katika dirisha dogo walimsajili Tariq Seif.
Hawakukosea kwani yeye ndie aliekua mstari wa mbele katika kuibakisha Biashara utd Ligi kuu huku akifunga mabao 7 katika mechi kumi.
AWAFUNGA STAND UTD YAMSAJILI.
Tariq Seif akiwa katika timu ya daraja la pili ya Transit Camp walikutana na Stand utd katika michezo miwili ya kirafiki katika dimba la Kambarage huku Tariq akifunga katika michezo yote miwili hivyo mashabiki wa Stand wakalazimisha usajili wake na hivyo viongozi wa Stand utd wakati huo kabla haijashuka daraja wakampa kandarasi.
AMTUNGUA MANULA, AMTIBULIA REKODI
Katika msimu wa 2017/2018 Stand utd walifanikiwa kulazimisha sare ya mabao matatu kwa matatu dhidi ya Simba katika uwanja wa Taifa.
Katika mchezo huo Aishi Manula alikua katoka kucheza michezo mingi ya Ligi bila ya nyavu zake kuguswa, na katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya mabao tatu kwa tatu Tariq Seif ndie alianza kufungua akaunti ya mabao kwa Stand baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi safi kutoka upande wa kulia.