Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars imefanikiwa kufika katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Challenge baada ya kutoka suluhu na Sudan katika mchezo wa mwisho wa kundi B.
Awali kabda ya mchezo Killi stars ilihitaji sare ya aina yoyote ile ama ushindi ili iweze kufuzu hatua ya nusu fainali, baada ya matokeo ya mchezo wa awali dhidi ya Zanzibar kupata alama tatu.
Stars sasa inaungana na kinara Kenya mwenye alama 9 kufuzu kutoka kundi B baada ya kukusanya alama 4 na kuwaacha Sudan wenye alama 2 na Zanzibar wenye alama 1 wakiyaaga mashindano hayo.
Baada ya sare ya leo sasa Stars inajiandaa kukabiliana na kinara wa kundi A Uganda katika hatua ya nusu fainali.