Kikosi cha Stars leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Taifa tayari kabisa kwenda kuandika historia mpya kwa Watanzania siku ya Jumapili kuelekea kufuzu Afcon 2019 nchini Misri.
Katika mazoezi hayo yaliyohudhuriwa pia na nyota wa zamani walioiwezesha Tanzania kufuzu katika Fainali za Africa mwaka 1980 nchini Nigeria ili kuwapa neno kidogo vijana wao.
Kina Iddi Pazi, Peter Tino na Athumani Chama walikuepo Taifa kuwapa maneno ya ushindi kina Msuva, Samata, Yondani na wenzie.
Tazama hapa picha jinsi hali ilivyokua katika uwanja wa Taifa.