Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera amekuwa akionekana sana hapa Tanzania kwa muda mrefu sana na kuzua maswali kwanini bado yupo Tanzania .
Kocha huyo ambaye watu wengi walitegemea muda huu angekuwa na timu ambayo angekuwa anaifundisha Lakini amekuwa akionekana sana hapa nchini.
Akizungumza na kituo cha habari cha Global Online TV ametoa sababu ya kwanini bado yupo Tanzania kwa muda mwingi .
“Siyo kweli kuwa niko Tanzania muda wote hapana , kuna muda huwa nasafiri sana naenda Nairobi , naenda Addis Ababa. Juzi Mimi na mdogo wangu tulienda Nairobi na Addis Ababa.
“Tunaondoka hapa Tanzania hata kwa siku mbili au wiki tunarudi tena Tanzania . Tunasafiri sana , kusema kuwa niko Tanzania muda wote huo ni uongo “- alisema kocha huyo mwenye asili ya Congo.
Pia kocha huyo aliweka wazi kuwa hawezi kuondoka Tanzania wakati hajamalizana na Yanga kutokana na pesa ambazo anawadai mpaka sasa hivi.
“Siwezi kuondoka Tanzania wakati Yanga nawadai , tuko kwenye mazungumzo mazuri na wao . Tutamalizana muda siyo mrefu “- alimalizia kocha huyo.
Alipoulizwa kuhusu suala la kufundisha timu nyingine alidai kuwa kwa sasa hawezi kuanza kufundisha timu nyingine kwa sababu anawadai Yanga hivo anasubiri amalizane nao.
“Hata nikikaa miaka mitatu bila kufundisha kwangu ni sawa kwa sababu ninafundisha timu ya Taifa ya Congo na ninalipwa vizuri .
“Siwezi kutafuta timu nyingine kwa sababu Yanga nawadai mpaka nitakapokuwa nimemalizana na Yanga ndipo nitakuwa na uwezo wa kutafuta timu nyingine ya kufundisha”- alimalizia kocha huyo