Wapwa, Awali kulikuwa na manung’uniko mengi kwamba njia iliyotumika kutoa taarifa za Simba Sc kumuacha kiungo wao Jonas Mkude haikuwa sahihi yaani ile ‘THANK YOU’.
Wengi walitoa mapendekezo yao kuwa kuna jambo lilipaswa kufanywa either katika mechi za mwisho za msimu angalau kumpa heshima ya utumishi wake uliotukuka ndani ya klabu.
Binafsi naunga mkono kuwa anapaswa kuagwa kwa heshima kwa kuwa ni mchezaji aliyecheza kwenye timu kwa muda mrefu na Mwanamapinduzi halisi wa sera za wachezaji wa timu za vijana kuunganisha na timu ya wakubwa na kisha kuaminika na kucheza kwa miaka mingi kupambana na wachezaji wa ndani na nje kwenye kugombea namba na kuwa mshindi.
Kote huku sina mashaka nako hata tone haikuwa jambo jepesi kukaa katika kikosi cha Msimbazi kwa miaka yote hiyo.
Sasa basi kwa kuliona hili ‘Wanalunyasi ‘ wamesema siku ya Simba Day watatumia fursa hiyo kumuaga Jonas Gerald Mkude. “Nungunugngu”.
Wapo sahihi kabisa kukawa nanyongeza ya kuistaafisha jezi yake, shughuli ikaanzia hapa maoni mengi, ila kwangu nikagundua kule si kuistaafisha ni kuiondoa kwenye mzunguko wa klabu na kwa muda waweza kusema kama kuipumzisha.
Kwa kuwa tumetariifiwa kuwa kama kuna mchezaji atapita njia ya Mkude kuja timu ya wakubwa basi atakabidhiwa yaani itarudi kwenye mzunguko.
Nimewahi kuona vilabu vikistaafisha jezi lakini huwa hairudi kwenye mzunguko wa klabu ni kwa maisha yote kama ambavyo jezi ya Marc Vivien Foe na Franco Bares pale AC Milan na kungineko.
Maana yangu kama unathamini hili ni lazima ufanye maamuzi magumu nadhani tunakumbuka ishu ya Mafisango pale Simba na taarifa za awali kuistaafisha jezi baadaye ikarudi tena kwenye mzunguko.