Kuna habari zilikuwa zimezagaa kuwa baadhi ya wachezaji wa Singida United wameandika barua kwa viongozi wao kuomba kuvunja mkataba kutokana na hali ngumu ya uchumi ndani ya klabu hiyo.
Kandanda.Co.Tz iliamua kumtafuta Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo Festo Sanga kutudhibitishia ukweli wa habari hizi ambazo zinazidi kuenea kwa kasi.
Alipotafutwa Kuzungumzia suala hili, Mkurugenzi huyo wa Singida United alisema hakuna barua yoyote iliyokuja katika ofisi za klabu hizo kutoka kwa baadhi ya wachezaji wakiomba kuvunja mikataba kwa sababu ya ukata.
Mwaka huu klabu hiyo ya Singida United ilikimbiwa na baadhi ya wachezaji kwa kile ambacho kinaonekana ni ukata mkubwa ndani ya klabu hiyo mpaka kufikia hatua ya kushindwa kuwalipa mshahara
Habari ambayo ilikuwa imezagaa jana
Rais wa klabu ya Singida United, Mwigulu Nchemba amekili kwa sasa Singida iko kwenye ukata kutokana Ligi kuu kutokuwa na mdhamini pia kumpoteza mdhamini mkuu wa klabu hiyo kampuni ya YARA na ndio maana waliamua kupunguza matumizi kwa kuwaacha baadhi ya wachezaji ambao walikuwa wanalipwa fedha nyingi, kandanda.co.tz imepata taarifa hizi kupitia Yossima Sitta Jr.
Mwigulu amedai wachezaji 6 ambao waliondoka sio tatizo kwao kwa sasa wanaendelea kujenga kikosi cha gharama dogo na wachezaji wazuri ambazo wataweza kuzimudu gharama zao na wameamua kuiga kwa klabu ya Mtibwa Sugar ambao wanakikosi cha ushindani na cha gharama ndogo.
–Kuhusu wachezaji waliondoka Rais Mwigulu amesema
“Batambuze alikuwa mchezaji mzuri ila alikuwa anataka mshahara wa milioni 7 na ada ya usajili ya milioni 90, Pia wakati timu ikishinda wachezaji walikuwa wanapewa bonasi ya laki moja yeye alikuwa anakataa anataka laki tano”
“Tulimruhusu Katsavairo aondoke kwa sababu alikuwa analipwa mshahara wa milioni 8, Kutinyu naye tuliachana naye kwa sababu ya kutaka mshahara wa milioni 7, Miraji Adam na Jamal Mwambeleko tumewaacha kwa sababu hawana moyo wa kuitumikia timu, Kazungu aliondoka kwa sababu ya kukosa nafasi ya kucheza”
Alisema Mwagulu
Pia alipoulizwa kuuhusu wachezaji watano Tiber John, Eliuter Mpepo, Kenny Ally, Salum Chuku na Swalehe Abdalah kuondoka Rais Mwigulu alisema
“Tiber John anaondoka anaenda nje kama alivyo Habib Kiyombo mabeki Salum Chuku na Swalehe wana madeko mengi tumewaruhusu waondoke, Mpepo na Kenny bado barua hazijanifikia ila kama zitanifikia tutazifanyia kazi Kwa sasa tutaandaa vijana wenye moyo wa kuitumikia Singida United kama Kennedy Juma” Alisema Rais Mwigulu.