Klabu ya Singida United yenye maskani yake mkoani Singida imeonyesha haina masishara katika kujiokoa na janga la kushuka daraja baada ya kufanya usajili wa nguvu ili kujinisuru.
Baada ya kuwasajili Haruna Moshi na Athumani Idd na kuanza kupata matokeo chanya ya kuanza kuvuna alama katika VPL sasa wamenogewa na kuamua kuongeza nguvu tena ili wasishuke daraja.
Singida United imewasajili kwa mkopo wa miezi sita Raphael Daud na Sospeter “Mwanza mwanza” kutoka Yanga sc ili aweze kuongeza nguvu katika eneo la kiungo na ulinzi huku Raphael Daud akienda kuungana na wakongwe Boban na Chuji katika eneo la kiungo.
Pia Singida imewasajili George Sangija na Aroon Lulambo “Makoena” wakitokea klabu ya mjini Dar es salaam ya KMC. Singida imewapata wachezaji hao kutoka KMC baada ya kuachwa na timu hiyo inayomilikiwa na manispaa ya Kinondoni.