Sambaza....

Timu mpya iliyopanda daraja msimu huu na kushiriki Ligi Kuu Bara Singida Big Stars imesema itaweka kambi nchini Tunisia ili kujiandaa na msimu ujao wa 2023/2024. 

Singida Big Stars imetangaza kuingia makubaliano ya ushirikiano na klabu ya US Monastir kutoka Tunisia na hivyo moja ya matunda ya ushirikiano huo ni kupata nafasi ya kujiandaa na msimu ujao nchini humo.

 

Kupitia taarifa rasmi ya klabu imesema watashirikiana na US Monastir katika kuendeleza vijana, ujuzi na uzoefu wa kitaaluma pamoja na usajili wa wachezaji.

” Maeneo tutakayoshirikiana ni pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu wa kitaaluma, usajili wa wachezaji, eneo la ufundi pamoja na kuendeleza timu zetu za vijana kupitia akademi ya Monastir,” ilisema taarifa hiyo.

Viongozi wa US Monastri pamoja na wenyeji wao Singida Big Stars.

Pia taarifa hiyo imeongeza kuwa kwa kupitia ushirikiano huo wamepata fursa yakuweka kambi yakujiandaa na msimu “pre season” nchini Tunisia kwa mualiko maalum wa US Monastir.

” Pamoja na mambo mengine tumepokea mualiko maalum yakuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya msimu 2023/2024 (pre season) nchini Tunisia kwa hisani ya washirika wetu US Monastir,” iliongeza taarifa hiyo.

Nyota wa Singida Big Stars.

US Monastir wapo kundi moja na klabu ya Yanga katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika na juzi wametoka kuwapa kipigo cha mabao mawili kwa sifuri na kulipa kisasi cha mchezo wa kwanza nchini Tunisia kwani na wao walipoteza kwa idadi hiyo ya magoli.

US Monastir ni klabu iliyoanzishwa tangu mwaka 1923 ikitumia uwanja wake wa nyumbani Stade Mustaph Bin Janet unaoweza kubeba watazamaji 15,000. Pia Monastir inamiliki klabu ya basketball. 

 

Sambaza....