Klabu ya Azam Fc imetangaza kuachana na baadhi ya wachezaji ambao walikuwa wanaitumikia klabu hiyo msimu uliopita.
Kwa mujibu wa mkuu wa idara ya habari wa Azam FC amedai kuwa wachezaji hao wamemaliza mikataba yao na uongozi wa klabu hiyo umedai hautoendelea nao.
“Nimepokea taarifa kutoka kwa viongozi wa juu kuhusu kuachana na wachezaji ambao wamemaliza mkataba na Azam FC”.
Mkuu huyo aliongeza kwa kuwataja wachezaji hao. “Wachezaji walioachwa ni Joseph Kimwaga, Hassan Mwasapili, Obrey Chirwa, Ramadhani Singano, Enock Atta Agey, Twafazwa Kutinyu, Steven Kingu na Danny Lyanga”.
Pia Azam FC imeachana na baadhi ya wachezaji ambao walikuwa chini ya umri wa miaka 20 walioenda kwa mkopo kwenye baadhi ya timu.
Mkuu huyo wa idara ametaja tarehe ya Azam FC kuingia kambi kwa ajili ya michuano ya Kagame.
” Tutaingia kambi tarehe 20 mwezi huu kwa ajili ya kujiandaa na kambi ya kujiandaa na michuano ya Kagame ambayo sisi ni mabingwa watetezi”.
“Tunajua hili kombe kubwa sana na kila timu inatamani sana kulibeba ila sisi tumejiandaa kùlitetea ,