Tayari bodi ya Ligi kupitia kikao kilichofanywa Jumapili wamekubaliana kumalizia raundi 10 za VPL zilizobaki kutokana na ugonjwa wa corona uliopelekea serikali kusimamisha shughuli zote zinazohusisha mikusanyiko ya watu.
TPBL inapendekeza katikati ya mwezi June Ligi ianze kuchezwa bila ya mashabiki huku pia ikuhudhuriwa na maofisa wachache na waandishi wa habari wachache kukiwa na tahadhari kubwa miongoni mwa timu shiriki. Lakini mapendekezo yote hayo yatategemea ruhusa ya serikali na hatua za kufuatwa kutoka kwa wizara zote husika.
Ikiwa Ligi itarejea kama kawaida baadhi ya timu za Ligi Kuu Bara ambazo zinamiliki wachezaji wa kigeni huenda zikapata tabu kutokana na baadhi ya makocha na wachezaji kutimka nchini na kwenda nchini kwao kujiunga na familia zao.
Kuna wachezaji na makocha wanaotoka nchi kama Ubeligiji, Burundi, Zimbabwe, Ghana, Msumbiji, Zambia, Uganda, Kenya na Rwanda ambazo katika nchi zao mipaka imefungwa ili kuzuia muingiliano wa watu ili kuthibiti ugonjwa wa corona.
Hivyo hata wakirudi nchini watachelewa kujiunga na wenzao moja kwa moja kutokana na kutakiwa kukaa kwa siku 14 karantini ili kuchekiwa kama hawana maambulizi ya virusi vya corona. Kutokana na athari hizo tazama nyota ambao huenda wakakosekana katika vikosi vyao.
Azam fc itawakosa
Bruce Kangwa, Donald Ngoma – Zimbabwe
Razack Barola, Yakubu Mohamed, Asamoah – Ghana
Nicholaus Wadada Uganda
Kocha Mkuu Aristica Cioaba
Simba sc itawakosa
Meddie Kagere – Rwanda
Francis Kahata – Kenya
Luis Miquissone – Msumbuji
Clatous Chama – Zambia
Sharaf Shiboub – Sudan
Yanga itawakosa
Kocha Mkuu Luc Aiymael.
Benard Morisson – Ghana
Si hizo timu tatu tuu ambazo zitaathirika lakini pia hata “Kino Boys” nao huenda wakawakosa baadhi ya nyota wao wanaotokea Burundi Jonathan Nahimana na Emmanuel Mvuyekure