Leo kulikuwa na mkutano wa waandishi wa Habari na klabu ya Simba ambapo msemaji wa klabu hiyo pamoja na mtendaji mkuu wa klabu hiyo walikuwa wamazungumza kuelekea kwenye mechi ya watani wa jadi, kwenye mkutano huo kuna mengi yamejitokeza.
Moja ya kitu ambacho mtendaji mkuu wa Simba alikitolea ufafanusi nitetesi za Rashid Juma kujiunga na majimaji FC “Kuna tetesi kwamba Rashid Juma amesajiliwa na timu ya daraja la kwanza, sio kweli. Rashid ni majeruhi na madaktari wa timu wanaendelea kumpatia matibabu.”- CEO Senzo
Kuhusu usajili wa dirisha dogo mtendaji mkuu amesema wiki watasajili à”Kabla hatujasajili tunahusisha wahusika wote. Tunafanyia kazi sana hilo. Tunategemea kabla ya wiki kuisha tutatangaza mchezaji mpya.”- CEO Senzo
Kuhusu mechi dhidi ya Yanga Haji Manara amedai kuwa wanaenda kupingana kwa alama tatu “Tumewafunga mara nyingi lakini hatuwezi kuwadharau japo sisi tumewazidi. Tunakwenda kupambana kutafuta alama tatu kama ilivyokuwa mechi ya jana ya Ndanda”- Haji Manara.
“2020 tunaanza na Yanga. Kama klabu tupo tayari, tupo tayari kwa maandalizi, tupo tayari kwa mchezo.”- CEO Senzo
Pia Simba wametoa utaratibu wa tiketi na wamedai wameanza kuuza tiketi Leo.”Tiketi zitaanza kuuzwa leo hivyo huna sababu kununua tiketi karibu na muda wa mchezo. Tununue tiketi mapema.”- Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki, Hashim Mbaga.
Jambo la Mwisho kwenye kikao hicho na waandishi wa Habari ni kuhusu Simba kuvunja mkataba na Mshambuliaji wao wa raia wa Brazil , Wilker Da Silva.