Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba wameanza kukiboresha kikosi chake kimyakimya kuelekea msimu ujao huku wakianza usajili katika eneo la ulinzi wa pembeni la kushoto anapocheza nahodha msaidizi Mohamed Hussein.

Simba inasemekana imeshanalizana na mlinzi wa kushoto wa Ihefu Fc Yahya Mbegu baada ya kumkosa katika usajili wa msimi uliopita. Mbegu atakwenda kupambania nafasi na Mohamed Hussein baada ya Gadiel Michael kushindwa kumpa changamoto ya kutosha mlinzi huyo wa Taifa Stars pia.

 

Awali Simba walikua wanamuhitaji kikosini Mbegu tangu msimu uliopita wakati akiitumikia Polisi Tanzania lakini kushidwa kufanya uamuzi kwa haraka kwa uongozi wa Simba kukawafanya Geita Gold kupita nae na kumsajili kabla ya kuachana nao na kutimkia Ihefu katika dirisha dogo.

Kiwango kidogo kinachoonyeshwa na Gadiel Michael ndio kilichowafanya viongozi wa Simba kutafuta mlinzi mwingine wa kushoto ambae atasaidiana na Tshabalala katika eneo la ulinzi wa kushoto wa timu hiyo.

Yahya Mbegu

Yahya Mbegu si mgeni katika klabu ya Simba kwani amewahi kupita hapo alipokua mchezaji wa Simba B, lakini baadae alitimka zake na kwenda Mwadui halafu Polisi Tanzania na sasa Ihefu.

Mlinzi huyo wa pembeni amekua katika kiwango kizuri katika michezo ya Ligi Kuu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaba na kumbuliaji akitumia akili nyingi ndani ya uwanja.

Sambaza....