Sambaza....

Simba wanashuka dimbani April 16 kuwakaribisha Yanga katika Dimba la Benjamin Mkapa wakihitaji ushindi kwa namna yoyote ile ili angalau kuwapoza mashabiki wake ambao wamekata tamaa ya ubingwa kutokana na kiwango kizuri cha Yanga.

Kuelekea mchezo huo kumekua na sintofahamu ya hali ya afya ya wachezaji wake watatu ambao wamekosekana katika michezo ya hivi karibuni kutokana na majeruhi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wachezaji wote wa Simba wameingia kambini tayari kujiandaa na mchezo huo hata Aishi Manula na Henock Inonga wameungana na wenzao licha ya kupata maumivu katika mchezi dhidi ya Ihefu.

“Kikosi kimeingia kambini asubuhi na leo jioni wataanza mazoezi ili kujiandaa na mchezo wa Jumapili dhidi ya Yanga. Wachezaji wote wapo kambini hata Manula na Inonga waliokua majeruhi,” Ahmed Ally alisema

Ahmed Ally pia amewatoa hofu mashabiki wa klabu ya Simba kuhusu kiungo wao Sadio Kanoute “Putin” ambae hajaonekana uwanjani katika mechi tatu mfululizo, mbilo dhdi ya Ihefu na moja ya ugenini dhidi ya Raja Casablanca.

Sadio Kanoute “Putin”

Ahmed Ally “Kanoute haumwi popote hakuonekana katika mchezo wa marudiano dhidi ya Raja Casablanca katika Ligi ya Mabingwa, hakuonekana uwanjani dhidi ya Ihefu katika mchezo wa FA robo fainali na ule wa Ligi lakini yupo fiti na haumwi popote atakuepo Jumapili.”

Kuelekea mchezo huo pia Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba Imani Kajuna ametangaza tiketi zitakazopatikana kuelekea mchezo huo, kama kawaida amesema kutakua na kifurushi cha ”Mnyama Package” ambazo zitauzwa kwa watu zaidi ya 20, pia kutakua na Executive tiketi pamoja na tiketi za Platinum. 

Sambaza....