Sambaza....

Unaweza kusema kama Simba sc wamekata kunyweshwa Lubisi (pombe maarufu ya wenyeji wa mkoa wa Kagera kutoka kwa wenyeji wao hao maarufu kama ”
“wanankurukumbi” baada ya kuwachapa mabao 2-0

Katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, uliofanyika leo hii kunako dimba la CCM Kaitaba ambapo mpaka timu zinakwenda mapumziko kulikuwa hakuna mbabe

Kipindi cha pili Simba sc walionekana kucharuka na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni kwa Kagera sugar, na kunafanikiwa kupata bao kunako dk ya 67, likifungwa na Said Ndemla kwa shuti kali nje kidogo ya lango la wapinzani wao.

Tano Bora ya Ligi Kuu Bara

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC2191534719432127305506
2Yanga SC2111464322359124235481
3Azam FC2131205340323155168413
4Kagera Sugar FC213617379178223-45256
5Tanzania Prisons211597775177207-30254

Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha zaidi Simba sc, na kuongeaza mashambulizi zaidi ambapo yalizaa matunda dk ya 80 baada nahodha John Raphael Bocco kuukwamisha mpira wavuni akimalizia kazi nzuri ya Shomari Kapombe aliyepanda upande wa kulia, bao hilo alifunga Bocco limfanya kuweka rekodi ya kumfuna mabao 10, golikipa Juma Kaseja hiyo ikiwa tangu alipokuwa achezea Azam FC huku Kaseja akichezea vilabu Simba, Yanga na Mbeya city

Kagera sugar walijitahidi kadri ya uwezo wao kupata angalau bao la kufutia machozi, lakini walinzi wa Simba walikuwa makini kuondosha hatari zote ambapo mpaka dk 90 zinakamilika Simba sc waliibuka na ushindi huo wa mabao 2-0

Kwa ushindi huo Simba sc sasa inarudi kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, baada kufikisha alama 32 huku wakiwaacha Azam FC kunako nafasi ya pili kwa alama zao 30

Kikosi cha Kagera sugar kilikuwa hivi
Juma Kaseja, Eladius Mfulebe, Adeyum Ahmed, Juma Nyosi, George Kavila, Pastory Athanas/ Edward Christopher dk 61, Ally Ufudu, Jaffary Kibaya, Ally Ramadhan na Atupele Green/ Peter Mwalyanzi dk 80

Simba sc
Aishi Manura, Nichoraus Gyan/ Shomari Kapombe dk 70, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei/ Laudit Mavugo dk 83, Said Ndemla, John Bocco, Shiza kichuya/ Mzamir yasin dk 88 na Emanuel Okwi

Sambaza....