Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba wameutumia uwanja wa nyumbani vyema baada ya kufuzu robo fainali kwa kishindo cha hali ya juu na kumaliza ndoto za Horoya kufuzu robo fainali.

Simba walikua na nia moja pekee kumfunga Horoya ili kuweza kufuzu robo fainali kwani ndio walikua washindani wao wakubwa kwa nafasi hiyo katika kundi lao. Sasa kwa ushindi huo wa mabao saba bila unawafanya kufikisha alama tisa na unawapeleka robo fainali wao na kinara Raja Casablanca.

 

Kalamu ya mabao ya Simba ilifunguliwa na Clatous Chama katika dakika ya tisa tu baada ya kupiga faulo iliyokwenda moja kwa moja na kutinga wavuni. Goli la pili la Simba lilifunga na Jean Baleke baada ya shuti kali la Kibu Denis  lililomshinda kipa wa Horoya na Baleke kuumalizia mpira.

Simba hawakuishia hapo kwani walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao matatu baada ya Clatous Chama kuandika bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Horoya kuunawa mpira uliopiwa na Shomary Kapombe katika dakika ya 35.

Clatous Chama

Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko ambapo Horoya waliwatoa wachezaji watatu kwa mpigo huku pia kipa alieanza Mohamed Kamar akitolewa kumpisha Silla ambae nae hakubadilisha chochote katika mchezo huo.

Dakika ya 54 Sadio Kanoute “Putin” alifunga bao la nne kwa kuupiga mpira kwenye kona “cave” na baada ya pasi nzuri kutoka kwa Chama. Jean Baleke alifunga bao lake la pili na la tano kwa Simba katika dakika ya 64.

Jean Baleke

Clatous Chama alihitimisha hatrick yake baada ya kufunga bao la tatu katika dakika ya 69 baada ya pasi safi kutoka kwa Pape Sakho aliyeingia uwanjani kuchua nafasi ya Kibu Denis

Sadio Kanoute alihitimisha ushindi mnono wa Simba kwa kufunga bao la saba na la mwisho kwa shuti kali nje kumi na nane na kufunga bao lake la pili katika mchezo.

Kwa ushindi huo sasa Simba wanafikisha alama 9 na kujitwaliwa nafasi ya pili nyuma ya  Raja Casablanca mwenye alama 13 baada ya kupata sare ya bao moja moja na Vipers. Horoya wamebaki na alama zao nne na Vipers wana alama mbili mkiani.

Clatous Chama akimgalagaza mlinzi wa Horoya na kufunga bao lake la tatu.

Simba sasa wameshafuzu kwenda robo fainali hivyo mchezo wa mwisho wa kundi lao dhidi ya Raja Casablanca ugenini utakua ni wakukamilisha ratiba.

Vikosi vya timu zote mbili vilivyokua!

Kikosi cha Simba!

1. Aishi Manula
2. Shomary Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Henock Inonga
5. Joash Onyango
6. Sadio Kanoute
7. Kibu Denis
8. Mzamiru Yassin
9. Jean Baleke
10. Saido Ntibazonkiza
11. Clatous Chama

Sub: Benno, Mwenda, Kenedy, Nyoni, Sakho, Bocco, Kyombo, Banda, Phiri

Kikosi cha Horoya

1. Mohamed Kamar
2. I Samake
3. K Diaw
4. S Koulibaly
5. M Fofana
6. Abdoulaye Faye
7. F Camara
8. D Kamara
9. N Soumah
10. M Wonkoye
11. P N’Diaye

Sub: Silla, Traore, Camara, Nikiema, Barry, Kante, Soumah, Doumbauya, Mangue Camara

Sambaza....