Uongozi wa klabu ya Simba leo umemteua na kumtangaza Mels Daalder Raia wa Uholanzi kuwa msaka vipaji (Skauti Mkuu) wa klabu kutokana na uzoefu wa kufanya skauti kwenye timu mbalimbali.
Mels ameshiriki kozi mbalimbali za duniani ikiwa ni pamoja na zilizoendeshwa na skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.
Mels ni mzoeefu na Tanzania kwani ameshawahi kuishi nchini pia ni shabiki mkubwa wa Simba. Mholanzi huyo pia ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na anaijua vizuri Ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla wake.
Mels ana uwezo wa kuongea lugha kadhaa ikiwemo Kiholanzi, Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili kwa kiasi fulani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema eneo la skauti ni muhimu ingawa lilikuwa haipewi nafasi kubwa na kwa kuliona hilo tumeamua kumleta Mels.
” Tunafuraha kubwa kumkaribisha Mels ili kuja kuboresha ufanisi kwenye skauti kwakuwa ni eneo muhimu katika mafanikio ya klabu yetu. Tunaendelea na maboresho muhimu kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa,” amesema Kajula.