Sambaza....

Tayari klabu ya Simba imetoa tamko rasmi wakisema watakwenda wapi kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao yaani “pre-season” kwa msimu wa 2023-2024.

Kupitia taarifa rasmi ya klabu Simba imeweka wazi watakwenda nchini Uturuki kujiandaa na msimu ujao ambapo watashiriki michuano mipya ya Super Cup Afrika.

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameweka wazi sababu za timu yao kwenda nchini Uturuki na si kubaki ndani ya nchi. Ahmed Ally alisema “Maswali ni mengi kwanini mnaenda Uturuki si mngebaki tuu kama wenzenu. Jibu ni kwamba hela ya kwenda Uturuki ipo tuu sio mpaka tuuze jezi.”

Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba Sc.

Ahmed amesema timu ambayo inashiriki michuano mikubwa ni lazima ijiandae kikubwa lakini pia wanawapa hadhi wachezaji kwa kufanya maandalizi makubwa.

“Pili timu ya inayoshiriki Super League lazima iwe tofauti na wengine. Tatu timu ya 9 kwa ubora Afrika lazima ifanye maandalizi sehemu kubwa kubwa. Nne wachezaji wetu wana hadhi ya Uturuki na Ulaya.

Halafu watu wa Uturuki wamefurahi kusikia tunaenda wamesema tumelipa heshima Taifa lao,” alimalizia Ahmed 

Sambaza....