Pamoja na kwamba wameshatwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa msimu huu wa 2017/18, Simba SC, wameendelea kuonesha lengo lao la kumaliza ligi hiyo bila kupoteza mchezo baada ya kuifunga Singida United kwa bao 1-0
Singida United, ilikuwa kunako dimba lake la nyumbani la Namfua Stadium iliruhusu bao hilo mnamo dakika ya 25, ya kipindi cha kwanza likifungwa na mlinzi wa Simba Shomari Salum Kapombe aliyeuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Singida United Ally Mustapha
Katika mchezo huo, uliotawaliwa zaidi na Singida United hasa kunako eneo la kiungo huku washambuliaji wake wakikosa maarifa ya kuipenya ngome ya Simba
Matokeo hayo, yanaifanya Simba izidi kupaa kileleni mwa jedwari la ligi hiyo kwa kufikisha alama 68, huku ikiwa imesaliwa na michezo dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba na Majimaji FC, ya Songea
Matajiri wa jiji la Dar es salaam, Azam FC, wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 52, huku Yanga SC wakishika nafasi ya tatu kwa alama zao 48