Sambaza....

Kocha mpya wa Simba sc, Pierre Lechentre, amekuwa na mwanzo mzuri baada ya kukiongoza kikosi chake hii leo kwa kuwacha Majimaji FC ya Songea kwa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi soka Tanzania bara

Simba 4 – 0 Majimaji

Kwa ushindi huo, unaifanya Simba kumaliza mzunguuko wa kwanza ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, ikiwa imekusanya jumla ya alama 35 baada ya kushuka dimbani mara 15

Katika mchezo huo, uliomuliwa na mwamuzi Erick Onoka kutoka Arusha huku akisaidiwa na kazi washika vibendera Mohammed Mkono kutoka Tanga na Arnold Bugado wa Singida, ambapo mpaka mapumziko Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yakifungwa na John Bocco “Adebayor”

Bocco aliipatia Simba bao la kwanza kunako dakika ya 15, akimalizia kazi nzuri ya beki Asante Kwasi, dakika chache baadae John Bocco aliipatia tena Simba bao la pili akimalizia klosi safi ya kiungo Saidi Ndemla

Bocco angeweza kufunga bao la tatu dakika ya 36, baada ya kugongeana vema na Emmanuel Okwi lakini shuti lake liliishia mikononi kwa golikipa wa Majimaji Saleh Malande, Lechantre alifanya mabadiliko ya kwanza kwa kumtoa Jamal Mwambeleko dakika ya 42 na nafasi yake ikachukuliwa na Mzamir Yasin

Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko kwa kumtoa Juuko Murshid na nafasi yake ikachukuliwa na kiungo James Kotei, mabadiliko hayo yalionekana kuinufaisha zaidi timu hiyo na dakika ya 53 Okwi aliipatia Simba bao la tatu akiunganisha vizuri mpira wa kona uliopigwa na Shiza Ramadhani Kichuya

Okwi tena aliipatia Simba bao la nne kunako dakika ya 69, lakini safari hii akimlamba chenga golikipa Saleh Malande baada ya kupokea pasi nzuri ya Bocco aliyekokota mpira kwa umbali mlefu kabla ya kutoa pasi hiyo akiwa ndani ya 18

Majimaji walikaribia kupata bao la kufutia machozi kunako dakika ya 75, baada ya mshambuliaji aliyetokea benchi Jerry Tegete kupiga mpira nje akipokea pasi ya Six Mwesekaga

Simba iliwakilishwa na

Aishi Manura, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Juuko Murshid/ James Kotei dk 47, Jonas Mkude, Jamal Mwambeleko/ Mzamir Yasin dk 44, Said Ndemla, Shiza Kichuya/ Laudit Mavugo dk 81, Emmanuel Okwi na John Raphael Bocco

Majimaji FC

Saleh Malande, Lucas Kikoti, Mpoki Makinyuke, Kennedy Kipepe, Paul Maona/ Alex Kondi dk 59, Hassan Hamis, Peter Mapunda/ Jerry Tegete dk 65, Yakub Kibiga, Geoffrey Mlawa/ Sixmund mwasekaga dk 68, Marcel Bonaventure na Jaffary Mohammed

Sambaza....