Sambaza....

Baada ya jana Yanga SC kuanza vyema ligi kuu Tanzania bara baada ya likizo fupi ya Corona kwa kuwachapa Mwadui FC goli 1-0 lililofungwa na Mapinduzi Balama, leo itakuwa zamu ya Simba SC.

Simba SC watawakaribisha Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa ambao wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani. Simba Sc watakuwa na swali kubwa la namna ambavyo wataanza ligi vyema kuelekea kuchukua ubingwa wao.

Kikosi cha Ruvu Shooting

Msemaji wa Ruvu Shooting , Masau Bwire amedai kuwa Simba SC watakufa kisayansi kwa sababu wana mikakati ya kisayansi katika kuiua Simba SC leo hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao huu wa kandanda.co.tz amedai kuwa wao wana mipango dhabiti. “Sisi tunampango wa kisayansi . Unajua sayansi haiongopi , kwa hiyo na sisi hatuna mipango ya kuongopa kwa sababu ya ukweli kuwa tutawafunga Simba Sc”. Alisema Masau Bwire.

Wachezaji wa Simba walishangilia goli lao dhidi ya Azam fc

“Mechi iliyopita walitufunga , ilikuwa ni mzigo mzito kwetu lakini tulijifunza . Unajua ukijifunza unakuwa na nafasi ya kutokosea tena kwa mara ya pili kwa sababu unakuwa unajua mbinu nzuri ili kutorudia makosa”- alimalizia Masau Bwire

Sambaza....