Sambaza....

Labda sijui mpira, mtanirekebisha. Simba na Yanga wangechukua mataji ya Afrika msimu huu, natazama fainali hapa. Hawa Wydad walikuwa wanafungwa mabao mengi Taifa kama Simba wangekuwa makini.

Away Simba hawakuwa na kipa mzoefu katika dakika 90 wala penalti. Yanga walizembea Taifa lakini ugenini USM Algier walilazimika kupiga fataki na kurudisha mipira mingi uwanjani kuwafanya Yanga wasipate bao la pili.

Mudathir Yahya Abas akimdhibiti kiungo wa USM Algier katika mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba ya Miquissone na Chama hawa Wydad wangetoka ile nusu fainali. Well, hata hii fainali kawaida sana kiaina katika quality. Hakuna ubora uliopitiliza.

Mtanirekebisha lakini kama Waarabu wakiendelea hivi wala hatupo mbali saaana kama nilivyokuwa nafikiria. Naruhusu maoni tofauti.

Katika fainali hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika Al Ahly achukua ubingwa baada ya kupata sare ya bap moja kwa moja ugenini dhidi ya Wydad na hivyo kumaliza kwa ushindi wa jumla wa mabao matatu kwa mawili baada ya mchezo wakwanza kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Eddo Kumwembe.

Sambaza....