Droo ya michuano ya kombe la FA maarufu kama Azamsports Federation Cup imefanyika leo katika studio za Azam Tv Tabata Jijini Dar es salaam na kuweka bayana nani kukutana na nani katika robo fainali na nusu fainali.
Michuano hiyo iliyobakisha hatua tatu pekee za robo fainali, nusu fainali na fainali kumpata mshindo tayari vimetajwa viwanja vitakavyotumika katika michezo ya nusu fainali na fainali.
Michezo ya robo fainali itakua ni kati ya Simba dhidi ya Ihefu na Azam Fc dhidi ya Mtibwa Sugar. Ambapo mshindi kati yao ndio watakutana nusu fainali.
Pia robo fainali nyingine inawakutanisha Singida Big Stars dhidi ya Mbeya City wakati Yanga watakutana na Geita Gold na mshindi kati yao ndio watakutana nusu fainali ya pili.
Michezo hiyo ya nusu fainalo itapigwa katika viwanja vya Nang’wanda Sijaona Mtwara na uwanja wa Liti mkoani Singida. Pia fainali za michuano hiyo mwaka huu zitafanyika Jiji la maraha Tanga katika Dimba la Mkwakwani.
Mshindi wa michuano hiyo ndio ataiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Hivyo ni wazi vilabu vya Azam Fc na Singida Big Stars vitaendelea kukabana koo ili kupata ushindi na kupata nafasi ya kuwakilisha nchi Kimataifa