Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ali amewaita mashabiki wa klabu ya Simba kuelekea mchezo wao Ligi ya Mabingwa Afrika huku akitangaza kupunguza viingilio katika mchezo huo kutokana na ushauri wa mwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji “MO”.

Ahmed Ali amesema miongoni mwa maeneo yakuimarisha uchumi wa klabu ni pamoja na viingilio vya mechi lakini pia mashabiki ni muhimu wakitokea uwanjani hivyo ndio maana wamesikia ushauri wa Mo Dewji na kupunguza viingilio.

“Shabiki namba moja wa klabu ya Simba alitushauri kamati tendaji baada ya kupanga viingilio kuelekea mchezo huo na kweli tulimsikiliza na kuvipunguza, sasa Mwanasimba atashindwa kuja uwanjani kwasababu zake zingine lakini sio kwakukosa kiingilio,” Ahmed Ali

Awali viingilio katika mchezo huo vilikua ni Mzunguko (5000), VIP B na C 20,000 na VIP A 30,000. Lakini viingio vipya sasa ni hivi hapa chini

Pia Ali Kamwe amewatoa hofu mashabiki wa klabu ya Simba na Watanzania kwa ujumla waliokua na wasiwasi wa timu yao kufanya vyema baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Horoya ugenini.

“Mchezo na Mbeya City unakua mgumu kuliko hata huu dhidi ya Raja, nina uhakika na ushindi dhidi ya Casablanca kuliko hata tungecheza na Mbeya City. Wachezaji wetu wanajua jinsi ya kucheza hii michezo, yaani mchezo ukiwa unaanza hawa kina Kapombe, Tshabalala wanakua ni mara kumi na moja zaidi ya uwezo wao,” Ahmed Ali afisa habari wa klabu ya Simba

Simba inaingia uwanjani siku ya Jumamosi kucheza dhidi ya Raja Casabanca katika mchezo wa kundi C ambao mchezo wakwanza Raja Casablanca walimfunga Vipers ya Uganda kwa mabao matano kwa sifuri na kuongoza kundi.

Sambaza....