Wekundu wa Msimbazi Simba sc wameendeleza moto wao katika dimba lá Taifa jijini Dar és salaam baada ya kuigaragazaa vibaya Stand UTD katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Ikicheza mbele ya mashabiki wake waliokua na shangwe ya hali ya juu baada ya kupatikana kwa boss wao Mo Dewji wachezaji wa Simba hawakuwaangusha baada ya kunogesha sherehe hiyo kwa ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.
Alikua ni Cleatus Cholla Chama alieandika bao katika dakika ya 30 katika kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Shiza kichuya upande wa kushoto. Chama alipokea mpira na kumpiga chenga mlinzi wa Stand United na “kucave” mpira upande wa kulia na kumuacha mlinda lango wa Stand Utd Mohammed Makaka akiwa hana lá kufanya.
Katika dakika ya 45 kuelekea kumaliza kipindi cha kwanza Emmanuel Okwi aliiandikia goli lá pili Simba baada ya kupokea pasi muruaa kutoka kwa Chola Chama na kuipeleka mapumziko Simba ikiwa mbele kwa mabao mawili.
Erick Mlilo alijifunga katika dakika ya 77 kutokana na mpira wa kona uliochongwa na Shiza Kichuya na kuifanya Simba kuandika bao la tatu la mchezo na mpaka mpira unamalizika Simba 3 na Stand UTD 0.
Kwa ushindi huo unaifanya Simba sc kufikisha point 17 na kushika nafasi ya tatu huku Stand Utd wakiwa nafasi ya 11 wakiwa na point 11. Lakini pia kitendo cha kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri ni kama wameilipa Yanga waliotoka kuwafunga watoto wa shule Allience School kwa mabao matatu kwa bila katika mchezo uliopigwa jana katika dimba lá Taifa.
Matokeo mengine ya michezo ya leo
Lipuli fc 0 Kagera Sugar 1
Selemani Mangoma 60′
Mbao fc 1 Mtibwa Sugar 0
Said Mussa JR .47′