Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba imesema itazindua jezi zake kwa namna ya kipekee kabisa mwaka huu wakishirikiana na Sandaland mdhamini wao kwa upande wa jezi msimu huu.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mtendaji wa klabu ya Simba wamesema watazindua jezi hizo katika kilele cha Mlima Kilimanjaro siku ya Ijumaa saa moja usiku.

“Jezi ya Simba itakwenda kuzinduliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro sehemu ya juu kabisa Barani Afrika,” alisema na kuongeza

“Jumatano safari ya kupata mlima Kilimanjaro itaanza na Ijumaa saa moja usiku ndio rasmi jezi ya Simba itazinduliwa hivyo Ahmed Ally anasafari yakwenda mlimani na Jumamosi jezi za Simba zitapatikana katika maduka yote ya jezi.”

Begi la jezi mpya za Simba msimu wa 2023-2024 zitakazozinduliwa mlima Kilimanjaro.

Nae Ahmed Ally akizungumzia tukio hilo la kihistoria kabisa nchini na Duniani amejinasibu yupo tayari kwa tukio hilo.

“Simba ndio klabu bora kabisa na mlima Kilimanjaro ndio sehemu ya juu Afrika hivyo vitu viwili bora kabisa vinakutana kileleni.”

“Hapa kwanza tutakua tumeua jiwe moja kwa ndege wawili, wakati dunia inashangaa jezi bora kabisa pia watapa fursa ya kuuona mlima Kilimanjaro hivyo tutakua tumeisadia serikali kwa asilimia 100 kutangaza utalii.
Tunajua hii haijawahi kufanyika duniani lakini sisi Simba tumefikiri hivyo na tutafanya.”

Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba Sc

Simba wamesema rasmi tarehe 21 jezi zao zitapatikana madukani kote na pia wametangaza siku itayofanyika Simba Day.

“Tamasha kubwa zaidi la soka Afrika litafanyika tarehe sita mwezi nane, hili ni tamasha la soka haswa sio vibonanza.

Tulitaka tufanye tarehe nane mwezi wa nane ambayo ndio tarehe rasmi yetu lakini ratiba ya Ngao ya Jamii kule Tanga imetubana maana tuna mechi na Singida tarehe 10 August.”

Sambaza....