Sambaza....

Uganda itakuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kanda ya CECAFA ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF 2023. Maamuzi hayo yalithibitishwa na CECAFA mnamo Jumatatu, Aprili 10, 2023 kupitia tovuti yao.

“Shirikisho la Vyama vya Soka Uganda (FUFA) limethibitisha kuwa mwenyeji wa michuano ya CECAFA Vijana U-15 na mechi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF kwa Ukanda wa CECAFA.” Ilisema taarifa hiyo.

 

Ingawa FUFA walikuwa wamethibitisha kuandaa Mashindano ya Wavulana U15, hawakuwa wametoa tamko lolote kuhusu kuandaa mashindano mengine. Sasa, kwa uthibitisho kutoka kwa CECAFA, Mechi za Kanda za kufuzu zinatarajiwa kufanyika kati ya Juni-Agosti.

Kampala Queens ambao hivi majuzi walishinda FUFA Women Super League watawakilisha Uganda wakiungana na Lady Doves na She Corporate ambao wameshiriki mara mbili katika misimu ya awali.

Simba Queens Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo

Vihiga Queens kutoka Kenya ilikua bingwa kwa mara ya kwanza mwaka 2021 huku Simba Queens ya Tanzania ikishinda mwaka jana. Ikumbukwe kwamba Mabingwa wa CECAFA hushinda tiketi pekee ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF.

Kwa upande wa uwakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo ambayo Simba ameshiriki mara mbilo mfululizo  bado hajapatikana kutokana na Ligi bado inaendelea na kukiwa na mchuano mkali kati ya vinara JKT  Queens wakifwatiwa na Simba Queens na Fountaine Gate Princess.

Sambaza....