Sambaza....

Baada ya kutesa katika Ligi Kuu Bara kwa kula viporo vyake safi na salama, sasa klabu ya Simba kuelekea nchini Algeria kuwafwata JS Souara katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kikosi cha Simba kitaondoka kesho Jumanne jioni kuelekea nchini Algeria kwa kupitia Dubai na kisha kuunganisha mpaka Algers nchini Algeria.

“Timu inaondoka kesho kupitia Dubai halafu tutachukua tena ndege ya kuelekea Algers. Hivyo ndio maana tunaondoka mapema ili tuwahi kufika kule. Inaeleweka kwa sasa kule kuna baridi kali na tumeshambiwa na waliotangulia kule.” Hajji Manara
Simba inatarajiwa kuondoka na msafara wa wachezaji 20 pamoja na viongozi na benchi la ufundi huku pia wakiambatana na baadhi ya mashabiki wachache ambapo msafara mzima hautazidi watu 50.

Simba inakwenda Algeria kwa tahadhari kubwa licha ya kuifunga JS Souara mabao 3 kwa sifuri jijini Dar es salaam lakini timu hiyo imekua ni tishio katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kutoka sare na Al-Ahly na kuifunga AS Vita.

Sambaza....