Simba sports club ya Tanzania wamesafiri na kuweka kambi nchini Uturuki, ambako watakaa huko kwa majuma kadhaa wakijifua na kujiandaa na msimu mpya wa mashindano wa 2023/24.
Msimu uliopita simba haikufanya vizuri katika mashindano waliyoshiriki ambapo kabla ya kuanza kwa msimu uliopita waliweka kambi nchini misri na kisha kwenda dubai katikati ya msimu katika dirisha la mapumziko la january.
Msimu huu simba imefanya sajili za wachezaji ili kuboresha mapungufu ya kikosi chao kabla ya msimu mpya wa mashindano kuanza. Simba ikiwa nchini uturuki itacheza michezo kadhaa ya kirafiki ikiwa ni sehemu ya kujiweka fiti na kukiandaa kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Mazingira ya kambi waliyopo simba ni mazuri yenye mahitaji yote ya msingi ya timu ikiwemo jimu za kisasa, Bwawa la kuogelea na viwanja vizuri vya mazoezi, isitoshe ni sehemu tulivu ambayo haijachangamana na makazi ya watu ko hakuna ghasia wala fujo kutoka kwa wakazi. Kwa mantiki hiyo utulivu wa kambi unalipa benchi la ufundi nafasi ya kuhuisha maarifa kwenda kwa wachezaji kikamilifu.
Licha ya hayo mwingine anaweza kuuliza, je hakuna maeneo mazuri nchini ambayo ni tulivu? Je hakuna maeneo yenye jimu za kisasa pamoja na mabwawa ya kuogelea? Kuna ulazima gani wa timu kwenda kuweka kambi nje ya nchi?.
Ni kweli yapo maeneo nchini yametulia na yenye kila hitaji la timu, hivyo hata kama simba wangeamua kubaki nchini bado wangejifua kikamilifu na kujiandaa barabara kuukabili msimu mpya wa mashindano. Lakini kuweka kambi nje ya nchi kuna faida nyingi ikiwemo hizi zifuatazo;
Kuongeza mashabiki
Simba inajulikana vema Tanzania na Afrika kutokana na ushiriki wake katika mashindano makubwa ya ngazi ya vilabu hivyo wanatembea nchi nyingi katika ushiriki wao hivyo wanajulikana. Kitendo cha kwenda kuweka kambi uturuki ni kupanua na kuongeza idadi ya mashabiki, pengine kuna wakazi watavutiwa na simba na wengine wanavutiwa nao lakini hawajawahi kuwaona hivyo wanatapata fursa kukutana na timu yao. Pili wapo watanzania ambao ni mashabiki wa simba ambao watausambaza utamaduni wa simba kwa wenyeji .
Kukuza mahusiano
Waneni husema “Undugu huanza kwa kutembeleana”. Ikiwa simba watacheza michezo kadhaa ya kirafiki wakiwa huko basi itazidi kupanua wigo wa mahusiano na vilabu vingine na kuongeza marafiki na hii itachagiza na kuongeza ushirikiano. Mahusiano yao yatasaidia kujifunza kati yao ni namna gani wanaziendesha timu na hata masuala ya kiutawala.
Kuikuza chapa ya simba kibiashara
Biashara ni watu, kujichanganya na watu kutaifanya biashara ikue na kujulikana kwa wateja ambao ni walaji kwa wingi. Simba kama taasisi inajiuza, simba kama chapa inajitembeza ili ionekane na kuvutia fursa kwa wawezekaji na wafanya biashara kuwekeza.
UKIONA VYA ELEA UJUE VIMEUNDWA