Sambaza....

Zana Coulibaly hili ni jina la mchezaji ambaye mashabiki wengi wa Simba huwa hawapendi kulisikia katika masikio yao. Ni jina ambalo wengi wanaamini lilpata bahati tu kusajiliwa Simba. Hana sura ya kuchezea Simba kabisa, hii ni kwa mujibu wa mashabiki wa Simba.

Mashabiki ambao wanaamini Simba siyo timu ya kawaida. Jezi ya Simba siyo ya kawaida kabisa, ndivyo wanavyoamini.

Jezi ambazo siyo za kawaida hazitakiwi kuvaliwa na mchezaji wa kawaida hata kidogo. Hapa ndipo ugomvi wa Zana na mashabiki wa Simba ulipoanzia.

Wanaamini kabisa Zana ni mchezaji wa kawaida sana. Na hakustahili kabisa kuja katika timu ya Simba, na cha ajabu kabisa hawakuona hata umuhimu wa kumpa muda Zana.

Hata jana jina lake lilipoonekana kama mchezaji ambaye angeanza kwenye mechi dhidi ya Al Alhly walianza kulaumu sana.

Waliamini kabisa kocha wa Simba ameweka mchezaji dhaifu kwenye mechi ngumu. Zana alikuwa haaminiki kabisa.

Nje ya uwanja alionekana mchezaji wa kawaida lakini ndani ya uwanja kulikuwa na matokeo tofauti kabisa.

Zana Jana alikuwa ni mchezaji muhimu kabisa katika mechi ya jana. Pamoja na kwamba kabla alionekana siyo mchezaji muhimu lakini jana alionekana ni mchezaji muhimu sana.

Kwanini ?, Zana jana alikuwa anakaba vizuri kwenye eneo lake. Alihakikisha katika eneo lake hakuna spaces (uwazi) eneo lake.

Eneo lake hakukuwepo na uwazi mkubwa ambao ungeleta madhara makubwa katika timu ya Simba.

Timu ilipokuwa haina mpira alihakikisha anakaba vizuri eneo lake na kutowapa nafasi wachezaji wa Al Alhly kushambulia kupitia eneo lake.

Timu ilipokuwa ina mpira Zana alikuwa anaisaidia sana timu kushambulia. Alipandisha timu kwenda juu na kurudi nyuma kuziba uwazi kwa haraka.

Alijaribu kupiga krosi katika lango la Al Ahly, hata goli la Simba yeye ndiye aliye tengeneza nafasi ya goli hilo, Krosi yake aliyopiga ilimfikia John Bocco na kutoa Pasi ya mwisho kwa Meddie Kagere.

Kwa hiyo kwa majukumu hayo mawili Zana , Jana aliibuka shujaa mbele ya midomo ya mashabiki wa Simba ambao wengi hawamwini.

Kuna wakati mwingine muda huwa ni mwamuzi mzuri , tunatakiwa kuvumilia na kusubiri muda utoe hukumu sahihi.

Sambaza....