Sambaza....

Mara baada ya Yanga sc kuangukia pua hapo jana kwa kukubali kichapo wakiwa nyumbani cha mabao 2-1 kutoka kwa Township Rollers, leo wawakilishi wengine kwenye michuano ya kombe la shirikisho hapa nawazungumzia wekundu wa msimbazi Simba sc, watashuka kwenye uwanja wa taifa kuwakaribisha Al Masri ya kutoka Misri

Kuelekea katika mchezo huo, binafsi nimekuwa na mawazo tofauti na kuamini Simba sc inaweza kupata ushindi wakiwa katika ardhi ya nyumbani japo haitakuwa kazi nyepesi hivyo wanapaswa kufanya kazi ya ziada, na hasa kuongeza umakini kwenye safu yao ulinzi ambayo imekuwa na makosa mengi

Yusuf Mlipili na Erasto Nyoni wamekuwa na tabia ya kukaba pamoja, hivyo kukosekana kwa mtu ambaye anaweza kumzunguuka mwenzake kimbinu ili kusahihisha makosa, pia wanakosa mlinzi kiongozi wa kuwakumbusha wenzake kurudi kwenye majukumu yao hivyo Simba wakifanikiwa kulisahihisha hili linaweza kuwasaidia kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.

Katika michezo ya aina hii, mara nyingi timu inapokuwa ugenini inakuwa na malengo ya kucheza kwa kujilinda sana huku wakishambulia kwa kushtikiza, kitu ambacho naamini Al Masry wanaweza wakakifanya lakini kwa aina ya makosa ambayo Simba wamekuwa wakifanya kwenye eneo lao la ulinzi yanaweza kuwasaidia Al Masry kumaliza mchezo wakiwa ugenini.

Mipira ya Kutengwa

Simba wanapaswa kuwa makini sana na aina hii ya mipira, Waarabu wanajua namna ya kuitafuta na kuitumia hasa wanapokuwa ugenini kujipatia mabao, hivyo Simba wanapaswa kuhakikisha wanajipanga kwa wakati na pre marking waifanye kwa usahihi

Ni wazi Simba wana safu nzuri sana ya ushambuliaji, inayoongozwa na John Bocco na Emmanuel Okwi hawa ni washambuliaji wenye uzoefu mkubwa na wanajua nini cha kufanya wanapokua kwenye eneo la mwisho, lakini wanapaswa kuongeza umakini zaidi wa kutumia nafasi chache watakazo tengeneza kwa maana katika michezo ya aina hii na ubora wa timu wanayocheza nayo wasitegemee kupata nafasi nyingi, hivyo endapo wakizitumia vizuri zinaweza kuwasaidia kuibuka na ushindi.

Al Masry wanaweza wasiishambulie sana Simba, lakini wakawa makini kwenye kutumia udhaifu wa Simba hivyo hii waichuke kama changamoto kuhakikisha wanaficha makosa na kufanya kazi ya ziada ili wafanikiwe kupata ushindi wakiwa nyumbani.

Kwenye eneo la kiungo huwa wanajitahidi kucheza vizuri, pia watatakiwa kupunguza pasi za nyuma na kuongeza ubora zaidi kwenye direct play ili kupata attacking play nzuri hii inaweza kuwasaidia kutengeneza nafasi za kufunga.

Pia wanapaswa kuiheshimu Al Masry kuwa ni timu nzuri na imekuja kwa lengo la kusaka matokeo, hata hotel waliyofikia inaweza kuwa somo kwa Simba la kutambua kuwa Masry wamekuja kazini hivyo mchezo hautakuwa mwepesi, hivyo wanapaswa kulitambua hili na kulifanyia kazi.

Sambaza....