Jumapili hii tunakwenda kushuhudia mpambano wa kukata na shoka kati ya Simba dhidi ya vibonde wao wa siku za nyuma Ruvu shooting. Kiukweli Simba sports amekuwa akipata matokeo mazuri mara kwa mara kwa Ruvu licha ya kupambana sana ndani ya game.
Japo kwa sasa ni tofauti kidogo wanakwenda kukutana wakiwa kwenye “memontum” ya aina yake baada ya’ kumdindia’ kigogo mwenzake Yanga kwenye mchezo uliopigwa Kigoma na kumalizika kwa suluhu.
Ni kweli “hakuna mbabe asiye na mbabe mwezie” huenda Simba wakawa wababe ya Ruvu kwenye mchezo huu lakini ni lazima afanye kazi ya ziada pia kwani ukiachilia nafasi zao kwenye msimamo mmoja yupo kwenye kuwania ubingwa moja yupo kwenye kujipambania na wimbi la kushuka daraja.
Ruvu yenye Kocha mzoefu na Charles Boniface Mkwasa master, anajivunia wachezaji nyota wenye uzoefu kama Buswita, Abdulhaman Musa, Haruna Chanongo, Japhary Mohamed na Marcel Kaheza huku wakichagizwa na chipukizi kama Nathaniel Chilambo na Rashid Juma.
Kwa upande wa wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club kuna taarifa za chini chini kwamba kuna mahusiano ‘dhaifu’ kati ya nyota kadhaa wa club hiyo na kocha Pablo Franco huku Clatous Chama akitajwa zaidi.
Hii inaweza kuwapa nguvu wapinzani wao Ruvu endapo ni kweli kutakuwa na msingano huo, kwa kuwa tunaamini kwenye umoja kama silaha ya ushindi.
Simba iliyoko kwenye nafasi ya pili ya msimamo ikiwa na alama 43 huku ikigubikwa na sare mbili mfululizo dhidi ya Yanga na Namungo.
Ni kama dhairi shahiri wameupoteza ubingwa wao walioutwaa msimu uliopita, hapa tunatakiwa kuangalia athari yake ni nini?
Huenda kibarua chake Pablo kikawa hatihati endapo wataunganisha dot za mafanikio na mwenendo wa timu chini yake.
Pablo ni muhimu sana kushinda game hii ili kujiweka salama kwenye vita vya kusitishiwa au kuendelea na mkataba ndani ya wekundu hao ambavyo vinaendelea sasa.
Ni muhimu Simba kushinda hii mechi ili kujikita sawia kwenye nafasi ya pili na kuwa na uhakika wa nafasi ya uwakilishi wa michuano ya kimataifa ambayo ni tofauti na majaliwa ya kufuzu kwa njia ya kombe la Azam federation Cup.
Nafasi ya pili pia ni muhimu kwa timu yeyote na hasa Simba endapo tutakubaliana kautema ubingwa kwa kuwa kuna kitita kikubwa cha fedha kwenye nafasi hivyo.
Mgawanyiko wa mapato toka Azam mwishoni mwa msimu ambapo
mshindi wa kwanza 500M
Mshindi wa Pili 250M
Mshindi wa tatu 225M