Klabu ya soka ya Simba rasmi imezindua kauli mbiu itakayotumika katika wiki ya Simba sambamba na kutaja timu watakayocheza nayo katika Simba Day.
Akizungumza na tovuti ya Kandanda.co.tz Imani Kajula amesema “Wiki ya Simba tumeibatiza kuwa ni wiki ya UNYAMA MWINGI,” na kuongeza “Wiki ya Simba, Unyama Mwingi, Simba Day, Unyama Mwingi. Unyama Mwingi inawasilisha mambo mengi ambayo yatatokea ndani ya wiki hii.”
“Niwashukuru washirika wetu wakubwa wa Simba Week na Simba Day, CRDB Bank lakini pia kuna washiriki wengine wakubwa wataingia.” Kajuna
Aidha pia msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally ametaja tarehe rasmi watakayozindua wiki ya Simba pamoja na kutaja timu watakayocheza nayo kutoka Zambia.
“Wiki ya Simba itazinduliwa na Matukio ni kama kuchangia damu, shughuliza kijamii kufanya usafi kwenye hospitali, masoko lakini pia tutakuwa na siku maalumu ya kutembelea mashujaa wa Simba.”
“Uzinduzi wa Simba Week tutafanya eneo la Buza Kanisani. Itakuwa tarehe 1, Agosti na tutaanza saa 4 asubuhi. Tunataka kufanya uzinduzi mkubwa na wa kihistoria. Wanasimba mjiandae. Simba Day tutacheza na bingwa kutoka Zambia, timu ya Power Dynamos. Huyu ndio tutacheza nae kwenye kilele cha Simba Week.” Ahmed Ally.
Pia uongozi wa Simba wamesema kambi inaendelea vizuri nchini Uturuki wachezaji wakiwa katika hali nzuri na wanatarajia kurudi nchini tarehe moja ya mwezi wa nane.
“Unyama Mwingi ni usajili mzuri, tamasha kubwa, kutimiza malengo ambayo tumejiwekea ya kuchukua mataji yote ya ndani na kufanya vizuri kimataifa.”
“Inshaalah timu itarudi kutoka Uturuki mapema August moja, waandishi mnakaribishwa uwanja wa ndege muwapokee wa Ulaya,” alimalizia Ahmed.