Sambaza....

Tunafeli darasa la saba, wenzetu wanafaulu kwenda kidato cha kwanza sisi tunaenda veta, wakifika kidato cha nne wanafeli rafiki zetu baadhi, wengine wanafauli kwenda kidato cha tano, waliofeli kidato cha nne wanaanza astashahda na waliofaulu wakifika kidato cha sita wengine wanafeli wengine wanaenda kuanza shahada, waliofeli wanaenda kuanza stashahada.

Huu ni mzunguko wa maisha kuyafikia mafanikio alieenda veta atakua fundi mzuri wa samani, atatengeneza samani za aliyefaulu chuo kikuu na kuwa meneja wa kampuni fulani wakati hawa waliofeli katikati kote kila mtu na darasa lake amejifunza na sasa amejitafuta amejipata sehemu akiwa kama meneja masoko mwenye stashahada, mtangazaji mwenye shahada mmoja, lazima mzunguko uendelee.

Yanga walifeli, wakajiuliza wakashika kalamu na karatasi wakarudi darasani kwa njia ingine Simba walifaulu mwanzo wa masomo wa ngazi za juu wameanza kwa kufeli hii haina maana wanapaswa kulia na kuweka kalamu chini, hapana wanatakiwa kuzichanga karata zao vyema, wajue walikosea wapi mbinu walizotumia kusoma kwa ajili ya mtihani wa awali zilikwama wapi, watakabiliana vipi na mtihani ujao ambao utaamua kuendelea na masomo ya juu zaidi au atarudia muhula, kurudia masomo kusubiri muhula ujao wa usaili? Ndio ni wakati wa Simba kupambania ndoto zao.

Simba hii si bora sana katika mapambano haya lakini mitihani waliyobaki nayo minne, basi mitatu kati yake inawezekana kabisa kufanya vizuri lakini kwa kuongeza juhudi na maarifa maradufu ya awali.

Mzamiru Yasin (katikati) akiwatambuka wachezaji wa Raja Casablanca

Simba wakawaheshimu Vipers hilo hawatakiwi kusahau lakini pia wawatumie wachezaji ambao katika nafasi mbili moja atafunga, John Boko si mchezaji mbaya ila ni mchezaji anaefunga nafasi chache kati ya nyingi anazopata.

Machanguzi yangu kwa Baleke na Phiri kama washambuliaji wawili watumike. Lakini pia chaguzi la kuanza Saido nyuma yao litakua bora zaidi. Muzamiru, Kanoute, wacheze katikati wakiwa na “wing back” Kapombe na Zimbwe.

Shomary Kapombe akimuacha mchezaji wa Raja Casablanca.

Mabeki watatu ndio chaguzi nzuri zaidi kwa mchezo huo, ili Simba akishambuliwa kuwe na mabeki watano na akishambulia awe na watu watano pia.

Inonga, Onyango na Kennedy wawe mbele ya Manula, nina uhakika Simba watarudi nyumbani na alama tatu.

Kila la kheri Simba, kila la kheri wenye nchi. Niwatakie Simba mitihani mema iliyobaki bado nina imani watafaulu.

Sambaza....