Sambaza....

Baada ya kelele nyingi kutoka kwa mashabiki wa Yanga kumtaka kocha wao mkuu Mwinyi Zahera kuwaachia timu yao, kocha huyo amedai kuwa yeye hakuajiriwa na mashabiki wa Yanga, Ila aliajiriwa na uongozi wa Yanga.

“Mimi sikuajiriwa na mashabiki wa Yanga, viongozi ndiyo niliosaini nao mkataba na siyo mashabiki wa Yanga. Siku viongozi wa Yanga watakaponiita na kunitaka niwaachie timu yao nitafanya hivo na sitoenda mazoezini”-alisema kocha huyo kutoka Congo.

Kuhusu kutojua kupanga kikosi imara, kocha huyo amejinadhibu kuwa yeye ni kocha mkubwa tena anayefundisha timu kubwa ya Taifa inayoshika nafasi ya tatu kwenye orodha ya ubora wa timu za Taifa Za CAF

“Ninafundisha timu ya Taifa ya Congo, timu ambayo inashika nafasi ya tatu katika orodha ya ubora ya CAF. Nimeenda AFCON ya tatu na mwakani naenda kufikisha AFCON ya nne , nafundisha wachezaji kutoka vilabu vikubwa kama Tottenham Hotspurs, Leo hii mtu anakuja kusema sijui kupanga kikosi”.

Kuhusu kufanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa , kocha huyo amedai kuwa hawana kikosi cha ligi ya mabingwa barani Afrika. “Tazama kwenye kikosi changu kuna mchezaji gani anayeweza kuingia kwenye kikosi cha Pyramid FC ?

“Wakati tunafanya usajili tulikuwa tunasajili wachezaji wa ligi kuu. Baada ya AFCON nilienda Paris kwa mapumziko nikaambiwa kocha unajua tutacheza Champions league ?. Wakati huo tulikuwa tumeshafanya usajili kwa ajili ya ligi kuu”.

“Hatukufanya usajili wa kushindana na Alhly au TP Mazembe. Kama tungefungwa na timu kutoka Burundi , Uganda ningeumia lakini kufungwa na timu kutoka Misri tena goli la pili kwa bahati mbaya basi kwangu ni hainiumi sana na wachezaji wamepigana sana.”

Kwa sasa kwenye klabu ya Yanga kumekuwa na hali ya hatari kutokana na mashabiki wa Yanga kushinikiza kocha mkuu wa Yanga kutoka baada ya kufanya vibaya katika michuano ya kimataifa kwa kufungwa na Pyramid FC kwa goli 2-1

Sambaza....