Sambaza....

Ilikuwa siku Jumapili moja tulivu sana nikiwa nimekwenda mapumziko na kumsalimia mjoma wangu mzee Msafili Ally Abdallah, anayeishi maeneo ya Kilosa mkoani Morogoro moja ya mikoa ambayo imekuwa ikitoa wachezaji wenye vipaji vikubwa sana vya soka

Tukiwa tumekaa sebuleni kwake huku akinisimulia mambo mengi yanayohusu soka, hasa lile soka la zamani enzi za akina Athumani Mambosasa, Juma Pondamali, Augustino Peter Magali “peter Tino” na wengine wengi ghafla tukaisikia taarifa ya usajiri ya beki Hassan Ramadhan Kessy akitokea Simba sc kwenda Yanga sc

Nikamalizia funda langu la juisi na kuanza kutafakari baadhi ya mambo, kubwa nikijiuliuliza namna gani Kessy anakwenda kwenye kikosi ambacho kwa nafasi anayocheza yeye tayari ina mfalme wake na yupo kwenye kiwango bora hapo namzungumzia Juma Abdul Jaffar

Ndio hakuna ubishi wakati Kessy anakwenda Yanga sc, Juma Abdul alikuwa kwenye kiwango bora na ilionekana ni ngumu kwa Kessy kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwa maana walikuwa wakipishana sana viwango vyao

Wakati ule Kessy alikuwa na matatizo mengi kwenye uchezaji wake, kuanzia kwenye majukumu ya msingi kwa ya ukabaji wake haukuwa wakulizisha sana lakini pia anapokwenda kwenye majukumu ya pili kuasidia mashambulizi Kessy hakuwa akifanya vizuri sana, klosi zake nyingi zilitoka nje ama kwenda kwenye miguu ya wapinzani

NIKAJIULIZA ATAWEZAJE KUMSHAWISHI KOCHA WA WAKATI ULE WA YANGA SC, HANS VAN DER PLUIJM.

Huku Juma Abdul akionekana kufanya vizuri sana kuanzia kwenye majukumu yake ya msingi ya ukabaji, pia anapokwenda kuasaidia mashambulizi klosi zake nyingi zilifika kwa walengwa na kuwa chanzo kikubwa cha mabao ya kina Amis Tambwe na Donald Ngoma

Nikajisemea moyoni ngoja nione vita ya mafahari wawili wa Morogoro, muda utasema

Maisha yanakwenda kasi sana na yanabadilika mithili ya taa za kuongezea magari, na ata mambo ndani ya Yanga sc yamebadilika Pluijm sio kocha wa Yanga kwa sasa yupo George Lwandamina kwenye nafasi hiyo, pia Hassan Kessy yule sio huyu wa sasa nimejaribu kumtazama kwa makini katika michezo mingi ya hivi karibuni kwenye akili na miguu yake kuna vitu vingi vipya

Hassan Kessy wa sasa anajua kukaba kwa umakini na utulivu mkubwa sana, lakini pia amekuwa msaada mkubwa kwenye mashambulizi ya Yanga, nikianzia kwenye mchezo dhidi ya St Louis kunako uwanja wa taifa alisababisha penati ambayo ilipigwa chongo na Obrey Chirwa

Pia katika mchezo wa marudiano kule Shelisheli alitengeneza nafasi 4 za kufunga ikiwemo ambayo Ibrahim Ajib alifunga huku moja akiipoteza, Papy Kabamba na Pius buswita nao walishindwa kuzitendea haki pasi zake

Kama hiyo haitoshi pia alikuwa chachu ya ushindi wa Yanga kule Songea dhidi ya Majimaji FC, kabla ya kuja kufunga mwenyewe jana katika mchezo dhidi ya Ndanda FC

Huyo ndiye Hassan Ramadhan Kessy wa sasa, licha ya kucheza kama mlinzi wa kulia lakini amekuwa akiingia kama kiungo mshambuliaji wa ziada (Invisible attacking midfielder)

Mwisho tu niseme hii ni changamoto mpya kwa Juma Abdul na taa ya kijani ilivyomwakia Hassan Kessy

Sambaza....