Shirikisho la soka nchini TFF limepitia uamizi wake wake wa kesi ya Feisal Salum uliofanyika January tisa mwaka huu na kati yake na klabu yake ya Yanga.
Awali Feisal Salum alitaka kuvunja mkataba wake na Yanga ili awe mchezaji huru lakini shauri lake lilipitiwa awali na kuonekana halina mashiko hivyo alipaswa abaki klabu yake ya Yanga.
“Baada ya kusikiliza mawakili wa pande zote mbili kamati imeona kuwa shauri hilo la mapitio (review) halina msingi wa kisheria kushawishi kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali na hivyo imetupilia mbali shauri hilo.” Taarifa kutoka TFF ilisema.
Aidha pia taarifa hiyo imesema sababu kwa undani zaidi kwenye shauri hilo itatolewa Jumatatu March 6 mwaka huu.
Feisal Salum tangu mwaka jana mwishoni hajaitumikia Yanga akishinikiza kuvunja mkataba wake. Mara ya mwisho Feisal kuitumikia Yanga ilikua katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri.