NAHODHA wa mabingwa mara mbili wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania Bara- Mtibwa Sugar FC, Shaaban Nditti amewaonyawachezaji wenzake nakuwataka kuhakikisha wanaongezaumakini kama timu ili kuwaondoa Northern Dynamo FC katika raundi ya awali ya michuano ya Caf Confederations Cup.
Mtibwa inarejea katika michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003 na Jumanne ijayo watakuwa Azam Complex Chamanzi kuwavaa wawakilishi hao wa Shelisheli kabla ya kurudiana mjini Roche Mahe Disemba 4.
” Tulihitaji nafasi hii na sasa tunapaswa kuonyesha uwezo wetu uwanjani.” anaanza kusema Nditti aliyedumu katika soka la ushindani kwa miongo miwili sasa huku akizitumikia klabu tatu tu ( Singida United 1999, Mtibwa 2000-2004, Simba SC 2004, Mtibwa 2005 hadi sasa)
” Umakini ni jambo muhimu sana kwetu kama kweli tunahitaji kufanya vizuri katika michuano hii.”. anaongeza, Nditti ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha mwisho cha Mtibwa kilichochapwa 3-0 na Santos FC ya Afrika Kusini katika michuano hiyo miaka 14 iliyopita.
” Tunapaswa kushinda nyumbani, kufunga magoli ya kutosha na kuzuia vizuri wasifunge na kupata goli/magoli ambayo yanaweza kutupa wakati mgumu katika mchezo wa marudiano.”