Sambaza....

Pale Hispania kunako klabu ya soka ya Real Madrid, kuna mlinzi wa kati kisiki ambaye anarekodi zake nyingi za ajabu na hata zenye kushawishi anaitwa Sergio Ramos.

Sio mgeni kwako kama ni mfuatiliaji mzuri wa michuano mikubwa  ya Kandanda kama Laliga, Klabu Bingwa Ulaya, EURO na kombe la Dunia, lazima utamuona akiwa ndani ya uzi wa Real Madrid ama ule wa timu ya Taifa la Spain huku akiwa na kitambaa cha unahodha kikiwa kimefungwa mkononi kwake.

Mwamba ni beki mmoja mtata sana, akili nyingi, nguvu kadhaa na ubishi kibao, kitasa kitasa kweli. Sasa kumbe jamaa ule utata wake wote ndani yake kuna asili na chembe chembe za ubabe na ugomvi wa Ng’ombe dume (Bull) unajua kwanini?

Mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos akimthibiti Messi Lionel wa Barcelona

Iko hivi, Ramos alipokuwa mdogo umri miaka 3-10, alikua akipenda sana kutizama michezo ya watu kupambana na Ng’ombe dume wao huiita (Bull fighting).

Huo ni mchezo wa kiasili ambapo mataifa kama Hispania, Ureno, Mexico na hata Ufaransa huicheza kwa wingi kwenye maonesho mbalimbali. Huletwa ng’ombe dume aliyenona ‘fahali’ na kupigana dhidi ya mtu mwenye mafunzo (bull fighter) na mwisho kupatikana mshindi, kati ya ng’ombe na binadamu. Vuta picha mziki wa mtu kupambana na ng’ombe😂, ni kifo njenje.

“Bull fighting” mchezo maarufu nchini Hispania na Mexico

Basi hio ndio ilikua ndoto ya maisha kwa Sergio Ramos, huku mama na baba yake wakimsihi kuacha kuupenda huo mchezo kwani ni hatari sana, yeye hakujali mpaka pale kaka yake aitwae Rene Ramos, ambeye ndiye wakala wake kwa sasa alipomkataza kuupenda mchezo huo na kumshauri kucheza soka.

Ramos alikubali kishingo upande akaanza kucheza mpira kunako klabu ya FC Camas kabla ya kujiunga na Sevilla kisha Real Madrid anakokipiga mpaka sasa, lakini bado kila akipata muda hupenda kutazama michezo hio hatari.

Sergio Ramos.

Kama aliwaza,akapenda na akaamini kuwa anaweza kupambana na Ng’ombe Dume aliyenona kabisa, utamwambia nini kuhusu Salah, Messi, Neymar, Mbappe, na wengineo?, Wacha watoto washike adabu😂.

Huyo ndio Sergio Ramos mwenye chembechembe za “Bull” na muweka rekodi mbaya na nzuri katika maisha yake ya soka.

Sambaza....