Kuna habari za kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kuonekana kumtaka Alexis Sánchez, mchezaji kutoka kwa hasimu wake mkubwa, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal FC).
Hii ni baada ya taarifa za awali kuonekana Manchester City kumwihitaji Alexie Sanchez tangu dirisha la usajili la majira ya joto na dirisha hili la majira ya baridi.
Ipi sehemu itakuwa na faida kwa Alexis Sánchez ?
Mpaka sasa Manchester City wana washambuliaji kama Sane, Raheem Sterling, Sergio Aguero, Gabriel Jesus.
Ongezeko la Alexis Sánchez linaweza kuonekana kama kuongeza upana wa kikosi cha Manchester City lakini kiuhalisia linaweza likaleta hali isiyo nzuri katika vyumba vya kubadirishia nguo kwa sababu Alexis Sánchez atakuja kuchukua nafasi ya mtu ambaye alionekana ana nafasi pia ndani ya kikosi.
Hali hii inaweza kuleta hali mbaya kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Manchester City wanatumia mifumo kama 3-5-2 na 4-3-3. Mifumo hii yote Alexie Sanchez anaweza akacheza vizuri.
Mfano kwenye mfumo wa 3-5-2 , Alexis Sánchez anaweza akacheza nyuma ya mshambuliaji.
Pia katika mfumo wa 4-3-3, anaweza ƙacheza kama false 9, na wakati mwingine kama mshambuliaji wa kati halisi. Hivo atatakiwa kupigana kumwondoa Aguero na Jesus.
Kwenye mfumo huu pia anaweza akacheza kama Winger , hali ambayo itamlazimu apambane kumweka benchi Raheem au Sane.
Hivo kwenda kwake Manchester City kutamfanya agombanie namba kwa kiasi kikubwa na siyo kuingia kwenye kikosi moja kwa moja kwa sababu wachezaji waliopo wamezoea mfumo wa Pep Guardiola kwa muda mrefu na wanafanya vizuri.
Vipi kuhusu Manchester United ?
Manchester United wana matatizo katika eneo la ushambuliaji, wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi lakini wanatumia chache.
Alexis Sánchez anauwezo wa kufunga kuanzia goli 20 ndani ya msimu mmoja.
Hii itakuwa moja ya tiba ya Manchester United ya kutotumia nafasi nyingi wanazotengeneza.
Hii ni faida ya kwanza ya Alexie Sanchez kupewa nafasi ya moja kwa moja kuingia kwenye kikosi cha Manchester United.
Kwenye dirisha kubwa la usajili , Manchester United walihusishwa na kumsajili Ivan Perisic lakini hawakufanikiwa kumpata.
Katika dirisha hili dogo ni ngumu kumpata Ivan Perisic kwa sababu upatikanaji wake ni mdogo ukilinganisha na Alexie Sanchez.
Alexie Sanchez anapatikana kwa urahisi sokoni, na anacheza kama Winger halisi.
Mpaka sasa Manchester United wamekuwa wakiwatumia washambuliaji wa kati kama kina Antony Martial na Marcus Rashford kama washambuliaji wa pembeni.
Hivo ujio wa Alexis Sánchez kutakidhi mahitaji ya Manchester United ya kumpata mshambuliaji halisi wa pembeni.
Hii pia itamsaidia Alexis Sánchez kuwa mtu ambaye ni chaguo la kwanza katika kikosi cha Manchester United kwa sababu mtu kama yeye anahitajika ndani ya kikosi.
Manchester United wameandaa kiasi kikubwa cha mshahara kwa Sanchez kuzidi Manchester City. Hii itakuwa na faida kwa Alexie Sanchez kama akiamua kwenda Manchester United.
Vipi kwa upande wa Arsenal itanufaika zaidi wapi ? Itanufaika zaidi Sanchez akienda Manchester United au Manchester City?
Jose Mourinho anataka kumpa Arsene Wenger pesa na Henrikh Mkhitaryan ambaye anaonekana hana nafasi katika kikosi cha Manchester United.
Hii itakuwa na msaada kwa Arsene Wenger ambaye ameandaa zaidi ya Euro 90 M kwa ajili ya kumsajili Thomas Lemar kama mtu wa kuja kuziba pengo la Alexis Sánchez.
Kumpata Henrikh Mkhitaryan kutampa nafasi ya kumpata mtu wa kuziba nafasi ya Alexis Sánchez.
Kwa hiyo, Alexis Sánchez kwenda Manchester United utakuwa uhamisho wenye faida zaidi kwa Alexis Sánchez, Manchester United na Arsenal.